Usawiri wa wahusika walemavu katika fasihi ya kiswahili

Date

2011

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu, umechunguza jinsi Wahusika wenye ulemavu walivyosawiriwa katika fasihi ya Kiswahili. Utafiti huu ulihusisha riwaya za Njozi Iliyopotea, Takadini na Nisamehe. Kwa kutumia nadharia ya Udenguzi, iliyoasisiwa na Derrida (1976), mtafiti alichunguza vipengele na misingi muhimu ya nadharia hii ambayo ilisaidia katika uchambuzi na uwasilishaji wa data husika. Utafiti ulihusisha sehemu za uwandani na maktabani ambapo data zilizopatikana zilichambuliwa kwa kutumia nadharia hiyo ya udenguzi. Maoni ya walemavu yalilinganishwa na jinsi waandishi walivyowatumia wahusika wenye ulemavu katika kazi za fasihi. Katika utafiti huu imeonekana kuwa, watu wenye ulemavu wanapata taabu katika jamii. Hii inatokana na ulemavu walionao. Kwa kuwa waandishi wa kazi za fasihi wanaandika yale yaliyomo katika jamii, ni wazi kuwa yale wanayoyaandika katika kazi za kifasihi hayana tofauti na yale yaliyomo katika jamii. Vilevile imebainika katika utafiti huu kuwa, watu wenye ulemavu hawakuwa na welewa wowote kuhusiana na jinsi wanavyotumika katika kazi za kifasihi, utafiti huu umewafungua macho na umewapa welewa na kuwapa mwanga wa nini kinaendelea katika fasihi ya Kiswahili. Imependekezwa katika utafiti huu kuwa, uchunguzi zaidi kuhusu watu wenye ulemavu unahitajika. Hasa walemavu wa aina nyingine na katika kazi nyingine za kifasihi kama vile tamthiliya na ushairi.

Description

Available in print form

Keywords

Swahili literature, Riwaya ya Nisamehe, Riwaya ya Takadini, Riwaya ya Njozi iliyopotea

Citation

Mukama, S.(2011) Usawiri wa wahusika walemavu katika fasihi ya kiswahili. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at (http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)