Athari za kiswahili katika msamiati wa kiwanji

dc.contributor.authorLusanjala, Sharon Umoti
dc.date.accessioned2019-11-27T16:32:34Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:42Z
dc.date.available2019-11-27T16:32:34Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:42Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.L87)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia Athari za Kiswahili katika Msamiati wa Kiwanji. Utafiti huu umefanyika wilayani Makete, Mkoa wa Njombe nchini Tanzania. Ili kufikia malengo yake, mbinu na njia mbalimbali za utafiti zikiwa ni pamoja na mbinu ya maktabani na uwandani zimetumika. Na njia zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni mahojiano pamoja na ushuhudiaji. Aidha, utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Makutano na Mwachano ya Giles na Byrne (1982), ambayo inaeleza kuwa lugha zinazokaribiana kimaeneo zinaweza kuathiriana. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa kuna athari mbalimbali za Kiswahili katika msamiati wa Kiwanji ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya msamiati wa Kiswahili katika Kiwanji, athari ya uchanganyaji lugha, upotoshaji wa matamshi sahihi ya msamiati wa Kiwanji, msamiati asilia wa Kiwanji kupotea, na msamiati wa Kiwanji kupungua matumizi. Vilevile, sababu zilizobainika ambazo huchangia athari hizi ni pamoja na mwingiliano wa kimatumizi wa Kiswahili na Kiwanji, baadhi ya maeneo kutozungumza Kiwanji, pia fahari ya kutumia Kiswahili kuliko Kiwanji, uhaba wa msamiati wa Kiwanji, na shughuli za kijamii na kibiashara. Mapendekezo yaliyotolewa ili kupunguza athari hizi ni pamoja na kuandaa makongamano na warsha mbalimbali za kuelimisha kuhusu umuhimu wa lugha za asili kama Kiwanji. Pia lugha ya Kiwanji ifanyiwe tafiti zaidi, ili iweze kuandikiwa kwa lengo la kusomwa na watu mbalimbali pamoja na kuitunza, kukipa Kiwanji dhima mbalimbali katika jamii, na kudumisha uhalisia wa lugha hiyo kwa kuzienzi mila na desturi.en_US
dc.identifier.citationLusanjala, S. U. (2014) Athari za kiswahili katika msamiati wa kiwanji, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3466
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectWanji languageen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectWanji (African people)en_US
dc.subjectLanguagesen_US
dc.titleAthari za kiswahili katika msamiati wa kiwanjien_US
dc.typeThesisen_US

Files