Uchunguzi wa athari za Kirombo katika jifunzaji wa kiswahili Vipengele vya kifonolojia na kimofolojia

No Thumbnail Available
Date
2015
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Suala la athari za L1 katika ujifunzaji wa Kiswahili kama L2 limewavuta wataalamu wengi. Hata hivyo, hakuna utafiti ambao umefanyika katika lugha ya Kirombo. Kwa hiyo utafiti huu ulichunguza athari za Kirombo katika ujifunzaji wa Kiswahili kama L2 kwa kubainisha athari, sababu za athari hizo na njia za kukabilia na athari hizo. Aidha, utafiti umefanyika katika kata za Mengwe Juu, Mengwe Chini, Manda Juu, Mamsera Juu, Mamsera Chini na Manda Chini, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Ili kufanikisha kazi hii, Nadharia ya Mwingiliano Lugha iliongoza utafiti huu, yaani ujipatajiwa L2 utawezekanaikiwanaikiwatumjifunzajianamwingilianowakaribunalughainayojifunzwa. Mbinu za utafiti zilihusu: usampulishaji, ukusanyaji, uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Data ya utafiti ni ya kutoka uwandani ambapo athari zilichambuliwa na kuwekwa katika makundi mawili; athari za kifonolojia na za kimofolojia kundi. Kazi imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza, imeeleza kiini cha utafiti na utaratibu uliozingatiwa katika kufanikisha utafiti. Sura ya pili, imeshughulikia mapitio ya maandiko kuhusiana na athari za L1 katika ujifunzaji wa L2. Mapitio haya yamebainisha kuwa athari za L1 katika ujifunzaji wa L2 zipo. Sura ya tatu, imehusu mbinu za utafiti ambapo populesheni, sampuli, usampulishaji pamoja na njia tatu za ukusanyaji data zilibainishwa. Sura ya nne, imeshughulikia uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Kwa ujumla data, iliyopatikana imechanganuliwa kwa njia ya maelezo na kanuni. Nadharia ya Mwingiliano Lugha ya Schuman (1978) ndiyo iliyoongoza mjadala na uchanganuzi wa data hii. Sura ya tano imeshughulikia matokeo, hitimisho, na tafiti fuatishi. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwepo kwa athari za kimatamshi 13 ambapo baadhi hutokana na kukosekana kwa sauti katika mfumo wa sauti za lugha ya Kirombo, na vighahiri. Pia, yamebainisha athari zinazotokana na utohoaji wa msamiati, na utofauti wa maumbo ya umoja na wingi ya ngeli kati ya Kirombo na Kiswahili, ambapo huleteleza athari za L1katika ujifunzaji wa L2 kama nadharia yetu invyodai kuwa, athariza L1 za kimatamshi, kitahajia, kisarufi na kimsamiati hujitokeza katika L2 wakati wa ujifunzaji. Pia, katika kufanya jitihada za matamshi ya L2, mwanafunzi huathiriwa na sauti zilizomo L1.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8702.M733)
Keywords
Swahili language, Morphology, Phonology, Rombo language
Citation
Mramba, P.T. (2015) Uchunguzi wa athari za Kirombo katika jifunzaji wa kiswahili Vipengele vya kifonolojia na kimofolojia, Tasnifu ya Uzamili (Kiswahili), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam