Usawiri wa mwanamke katika nyimbo za ngoma ya mganda ya Wanyasa.

dc.contributor.authorChitimbe, Barnaba
dc.date.accessioned2019-10-26T08:26:14Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:42Z
dc.date.available2019-10-26T08:26:14Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:42Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8593.C475 )en_US
dc.description.abstractUtafiti huu uliazimia kutimiza lengo kuu ambalo lilikuwa ni kubainisha jinsi dhamira za nyimbo za ngoma ya Mganda ya Wanyasa zinavyomsawiri mwanamke. Katika utafiti huu nadharia za ufeministi na uhalisia zilitumika sambamba na mbinu ya ushuhudiaji na mahojiano katika kukusanya data. Aidha uchambuzi wa data uliongozwa na mkabala wa kitaamuli kwa kiasi kikubwa na takwimu zilitumika pale tu zilipohitajika.Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba nyimbo za ngoma ya Mganda ya Wanyasa zimemsawiri mwanamke katika mtazamo hasi na chanya. Katika mtazamo chanya mwanamke ameelezwa kuwa na thamani kubwa kutokana na kuwa mchapakazi hodari, mshauri mzuri katika jamii, mvumilivu na kama mama na mlezi mzuri wa watoto. Katika mtazamo hasi, mwanamke ameelezwa kuwa ni kiumbe anayenyanyasika na kugandamizwa katika jamii kwani jamii inamchukulia mwanamke kuwa ni mtu asiye na haki mbele ya mwanamume, mtu mwenye wivu, mshirikina, malaya, mtu wa kukaa nyumbani na ni kiumbe tegemezi kwa mwanamume. Mwisho hitimisho la utafiti limedhihirisha kwamba jamii inapaswa kuelimishwa ili kuacha kumkandamiza mwanamke pamoja na kuondoa mtazamo hasi dhidi ya mwanamke.en_US
dc.identifier.citationChitimbe, B,(2014) Usawiri wa mwanamke katika nyimbo za ngoma ya mganda ya Wanyasa,Master dissertation, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3468
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectNyanja languageen_US
dc.subjectNyasa (African people)en_US
dc.subjectWomen in Literatureen_US
dc.subjectNyasa (African people)en_US
dc.titleUsawiri wa mwanamke katika nyimbo za ngoma ya mganda ya Wanyasa.en_US
dc.typeThesisen_US

Files