Usawiri wa mwanamke katika nyimbo za ngoma ya mganda ya Wanyasa.

Date

2014

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu uliazimia kutimiza lengo kuu ambalo lilikuwa ni kubainisha jinsi dhamira za nyimbo za ngoma ya Mganda ya Wanyasa zinavyomsawiri mwanamke. Katika utafiti huu nadharia za ufeministi na uhalisia zilitumika sambamba na mbinu ya ushuhudiaji na mahojiano katika kukusanya data. Aidha uchambuzi wa data uliongozwa na mkabala wa kitaamuli kwa kiasi kikubwa na takwimu zilitumika pale tu zilipohitajika.Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba nyimbo za ngoma ya Mganda ya Wanyasa zimemsawiri mwanamke katika mtazamo hasi na chanya. Katika mtazamo chanya mwanamke ameelezwa kuwa na thamani kubwa kutokana na kuwa mchapakazi hodari, mshauri mzuri katika jamii, mvumilivu na kama mama na mlezi mzuri wa watoto. Katika mtazamo hasi, mwanamke ameelezwa kuwa ni kiumbe anayenyanyasika na kugandamizwa katika jamii kwani jamii inamchukulia mwanamke kuwa ni mtu asiye na haki mbele ya mwanamume, mtu mwenye wivu, mshirikina, malaya, mtu wa kukaa nyumbani na ni kiumbe tegemezi kwa mwanamume. Mwisho hitimisho la utafiti limedhihirisha kwamba jamii inapaswa kuelimishwa ili kuacha kumkandamiza mwanamke pamoja na kuondoa mtazamo hasi dhidi ya mwanamke.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8593.C475 )

Keywords

Nyanja language, Nyasa (African people), Women in Literature, Nyasa (African people)

Citation

Chitimbe, B,(2014) Usawiri wa mwanamke katika nyimbo za ngoma ya mganda ya Wanyasa,Master dissertation, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.