Matumizi ya taswira katika nyimbo za sherehe za jando na unyago: jami1 ya wamwera

Date

2012

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam,

Abstract

Lengo la utafiti huu lilikuwa kufafanua matumizi ya taswira katika nyimbo za sherehe za jando na unyago za jamii ya wamwera. Lengo hili limeweza kufanikiwa kutokana na kukamilika kwa malengo mahsusi yaliyohusu kubainisha taswira zinazazojitokeza katika nyimbo hizo na kueleza umuhimu wa taswira hizo. Maandiko na machapisho mbalimbali kuhusu nyimbo, na mahususi nyimbo za jando na unyago, yamepitiwa yakiongozwa na nadharia ya simiotiki Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, nyimbo za jando na unyago za jamii ya wamwera hutumia taswira mbalimbali zinazofungamana na utamaduni wa jamii hiyo. Nyimbo hizi hubeba ujumbe mbalimbali si tu kwa wahitimu wa jando na unyago bali pia kwa jamii nzima ya Wamwera Mwisho tumetoa hitimisho kuu la utafiti, lililoainisha maeneo mbalimbali ya kufanyia utafiti katika nyimbo za jando na unyago za wamwera

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8539.M33)

Keywords

Mwera Language, Tanzania

Citation

Mahundi, S (2012) ,Matumizi ya taswira katika nyimbo za sherehe za jando na unyago: jami1 ya wamwera, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam