Matumizi ya lugha ya Kiswahili na utambulisho wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, wilaya ya Kahama, Tanzania

dc.contributor.authorMhango, Pauline
dc.date.accessioned2019-10-07T13:13:29Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:42Z
dc.date.available2019-10-07T13:13:29Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:42Z
dc.date.issued2013
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu matumizi ya Kiswahili na utambulisho wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi. Utafiti huu ulikuwa na malengo manne yaani kubainisha msamiati unaotumiwa kuwatambulisha wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, kufafanua muundo wa msamiati, kubainisha na kuchambua misemo inayowatambulisha wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi na kueleza sababu za kutumia msamiati na misemo inayowatambulisha kama kundi moja la wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi tofauti na makundi mengine ya kijamii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi wanatumia msamiati wa Kiswahili wa kubuni, uchanganyaji wa maneno ya lugha mbili, utumiaji wa maneno yaliyofupishwa, finyazo na lakabu. Msamiati wa Kiswahili cha wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi una muundo unaopachika viambishi mwanzoni na mwishoni mwa mzizi, muundo wa ufupisho wa maneno, muundo wa maneno mawili au zaidi na muundo unaotokana na uradidi. Matokeo ya utafiti huu pia yanaonesha kuwa wafanyakazi wa mgodi huu wanatumia misemo inayoakisi hali mbalimbali za kijamii kusawiri mamlaka, hadhi na kadhalika. Aidha, wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi wanatumia aina ya Kiswahili ili kujenga mshikamano na umoja, kupamba mazungumzo, kuficha siri, kujigamba na kupinga maamuzi wasiyokubaliana nayo kuhusu utaratibu na mpango wa kazi.en_US
dc.identifier.citationMhango, P (2013) Matumizi ya lugha ya Kiswahili na utambulisho wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, wilaya ya Kahama, Tanzania, Tasinifu ya M.A. (Kiswahili), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3470
dc.language.isootheren_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectBuzwagien_US
dc.subjectKahama districten_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleMatumizi ya lugha ya Kiswahili na utambulisho wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, wilaya ya Kahama, Tanzaniaen_US
dc.typeThesisen_US

Files