Matumizi ya lugha ya Kiswahili na utambulisho wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, wilaya ya Kahama, Tanzania

Date

2013

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu unahusu matumizi ya Kiswahili na utambulisho wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi. Utafiti huu ulikuwa na malengo manne yaani kubainisha msamiati unaotumiwa kuwatambulisha wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, kufafanua muundo wa msamiati, kubainisha na kuchambua misemo inayowatambulisha wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi na kueleza sababu za kutumia msamiati na misemo inayowatambulisha kama kundi moja la wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi tofauti na makundi mengine ya kijamii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi wanatumia msamiati wa Kiswahili wa kubuni, uchanganyaji wa maneno ya lugha mbili, utumiaji wa maneno yaliyofupishwa, finyazo na lakabu. Msamiati wa Kiswahili cha wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi una muundo unaopachika viambishi mwanzoni na mwishoni mwa mzizi, muundo wa ufupisho wa maneno, muundo wa maneno mawili au zaidi na muundo unaotokana na uradidi. Matokeo ya utafiti huu pia yanaonesha kuwa wafanyakazi wa mgodi huu wanatumia misemo inayoakisi hali mbalimbali za kijamii kusawiri mamlaka, hadhi na kadhalika. Aidha, wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi wanatumia aina ya Kiswahili ili kujenga mshikamano na umoja, kupamba mazungumzo, kuficha siri, kujigamba na kupinga maamuzi wasiyokubaliana nayo kuhusu utaratibu na mpango wa kazi.

Description

Keywords

Swahili language, Buzwagi, Kahama district, Tanzania

Citation

Mhango, P (2013) Matumizi ya lugha ya Kiswahili na utambulisho wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, wilaya ya Kahama, Tanzania, Tasinifu ya M.A. (Kiswahili), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)