Hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya mifugo Ndugu Herman K. D. Kirigini (MB) akifungua Mkutano wa kumi wa kisayansi wa chama cha uzalishaji mifugo Tanzania katika ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano - Arusha Tarehe 18 Octoba, 1983
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Ninayo furaha kubwu mno kupata fursa hii kwa mara nyingine tena kuwa parmoja nanyi katika sherehe hii ya kufungua mkutano huu ambao ni wa kumi wa Chama cha Uzalishaji Mifugo Tanzania (Tanzania Society of Animal Production) Kwa uhakika naweza kutamka kuwa furaha yangu leo hii ni furaha yenu pia kwani Chama chetu sasa kina umri wa miaka kumi tangu kuanzishwa mwaka 1973. Katika kikao hiki mtapata fursa ya kutafakari mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Napenda vile vile kutumia nafasi hii ya mwanzo kuwakaribisha hapa Arusha na hasa katika kikao hiki wageni wote wanaotoka nje na ndani ya nchi yetu, wataalamu wa fani na taaluma mbali mbali za mifugo, wafugaji kutoka vijijini, maafisa wa mifugo kutoka wizarani, mikoani na wilayani na wengine wote.