Matumizi ya Kiswahili vijijni na hatima yake kwa lugha ya Kibena, nchini Tanzania

dc.contributor.authorMkungilwa, Tiem
dc.date.accessioned2021-04-12T15:14:55Z
dc.date.available2021-04-12T15:14:55Z
dc.date.issued2016
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8701.M58)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umechunguza matumizi ya Kiswahili vijijini na hatima yake kwa lugha ya Kibena, nchini Tanzania. Malengo makuu ya utafiti huu yalikuwa kubainisha makundi ya wazungumzaji wa lugha ya Kibena, kubainisha maneno yanayotumia Kiswahili na maeneo yanayotumia lugha ya Kibena na kujadili matumiza ya Kiswahili vijijini ili kuelezea hatima ya Kibena. Ili kufikia malengo hayo, utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uchanganuzi wa kimaeneo iliyoasisiwa na Fishman (1972). Nadharia hii inaeleza mazoea ya wazungumzaji ya kupenda kuchagua kutumia lugha fulani katika eneo fulani na lugha nyingine itumike katika eneo jingine. Mtafiti alitumia mbinu za hojaji na mahojiano wakati wa ukusanyaji data na kufafanuliwa kwa njia ya kimaelezo na kiidadi. Watafitiwa 144 walishiriki katika utafiti huu ambapo usampulishaji nasibu tabakishi ulitumika katika vijiji vya Itipingi, Kichiwa na Itunduma. Utafiti huu umebaini kwamba idadi ya watafitiwa wanaotumia Kiswahili ni kubwa kuliko wanaotumia lugha ya Kibena. Matokeo yanadhihirisha kuwa katika maeneo ya nyumbani , majirani, sokoni, misibani, kanisani, harusini na kazini, Kiswahili kinatumiwa na wazungumzaji wengi kuliko Kibena. Aidha lugha ya Kibena imeonekana kutumiwa zaidi na wazee, wanawake na wasiosoma shule katika maeneo ya nyumbani, majirani, msibani na kazini. Matokeo haya yanaonesha kwamba lugha ya Kibena iko hatarini kutoweka kwa sababu wazungumzaji wa Kibena wanaendelea kupungua. Mwisho, utafiti huu unapendekeza kwamba watafitiwa wengine wanaweza kufanya tafiti nyingine, ili kuchunguza kuweka kwa lugha ya Kibena na athari zake kwa utamaduni wa jamii ya Wabenaen_US
dc.identifier.citationMkungilwa, T (2016) Matumizi ya Kiswahili vijijni na hatima yake kwa lugha ya Kibena, nchini Tanzania, Masters dissertation,University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15082
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectBena languageen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleMatumizi ya Kiswahili vijijni na hatima yake kwa lugha ya Kibena, nchini Tanzaniaen_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Tiem Mkungilwa.pdf
Size:
178.12 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: