Matumizi ya Kiswahili vijijni na hatima yake kwa lugha ya Kibena, nchini Tanzania
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umechunguza matumizi ya Kiswahili vijijini na hatima yake kwa lugha ya Kibena, nchini Tanzania. Malengo makuu ya utafiti huu yalikuwa kubainisha makundi ya wazungumzaji wa lugha ya Kibena, kubainisha maneno yanayotumia Kiswahili na maeneo yanayotumia lugha ya Kibena na kujadili matumiza ya Kiswahili vijijini ili kuelezea hatima ya Kibena. Ili kufikia malengo hayo, utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uchanganuzi wa kimaeneo iliyoasisiwa na Fishman (1972). Nadharia hii inaeleza mazoea ya wazungumzaji ya kupenda kuchagua kutumia lugha fulani katika eneo fulani na lugha nyingine itumike katika eneo jingine. Mtafiti alitumia mbinu za hojaji na mahojiano wakati wa ukusanyaji data na kufafanuliwa kwa njia ya kimaelezo na kiidadi. Watafitiwa 144 walishiriki katika utafiti huu ambapo usampulishaji nasibu tabakishi ulitumika katika vijiji vya Itipingi, Kichiwa na Itunduma. Utafiti huu umebaini kwamba idadi ya watafitiwa wanaotumia Kiswahili ni kubwa kuliko wanaotumia lugha ya Kibena. Matokeo yanadhihirisha kuwa katika maeneo ya nyumbani , majirani, sokoni, misibani, kanisani, harusini na kazini, Kiswahili kinatumiwa na wazungumzaji wengi kuliko Kibena. Aidha lugha ya Kibena imeonekana kutumiwa zaidi na wazee, wanawake na wasiosoma shule katika maeneo ya nyumbani, majirani, msibani na kazini. Matokeo haya yanaonesha kwamba lugha ya Kibena iko hatarini kutoweka kwa sababu wazungumzaji wa Kibena wanaendelea kupungua. Mwisho, utafiti huu unapendekeza kwamba watafitiwa wengine wanaweza kufanya tafiti nyingine, ili kuchunguza kuweka kwa lugha ya Kibena na athari zake kwa utamaduni wa jamii ya Wabena