Unyambulishi wa vitenzi katika lugha ya Runyankore.
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Kazi hii ililenga kuelezea uliyambulishi wa vitenzi katika Runyankore kwa kuchunguza mofimu za Utendea, Usababishi, Utendana, Utendeka na Utendwa. Mkabala wa ufafanuzi ndio umetumiwa kubainisha mofimu hizi, rnfuatano na kanuni zinazotawala pamoja na vipengele vya kiisimu vinavyojitokeza katika mchakato wa unyambulishi. Nadharia mbili zimetumiwa kwa pamoja Kiolezo Good (2007) na Kanuni ya Kioo Baker (1985) kuelezea unyambulishi katika lugha ya Runyankore. Kiolezo cha Mame- Bantu UTTU kama kilivyopendekezwa na Hyman (2003a) ndicho kimetumiwa kudhihirisha kuwa kuna mpangilio maalum wa mofimu nyambulishi katika lugha za Kibantu. Kanuni ya Kioo kulingana na Baker (1985) ni kanuni ya sarufi majumui inayopendekeza kuwa minyambuliko ya kimofolojia ni lazima iakisi minyarnbulika ya kisintaksia na kinyume chake. Kuwa hivyo, tokeo la kimofolojia lilitokana na masharti ya Kiolezo na Kanuni ya Kioo. Moflmu nyambulishi zinazoweza kuelezwa vizuri na Kanuni ya Kioo zimeelezwa na zile ambazo haziwezi zimeelezewa na Kiolezo. Matokeo yameonesha kuwa, unyambulishi wa vitenzi katika Runyankore unahusisha mizizi ya vitenzi ambapo mofimu nyambulishi hupachikwa, Mofimu nyambulishi hizi pia zilionesha tabia ya mofimu mbili au tatu kuambatana katika mzizi wa kitenzi kwa kufuata kanuni. Aidha, michakato mingine ya kiisimu inayojitokeza katika mchakato wa unyambulishaji imeelezwa na namna inavyojitokeza. Mwishowe, tumependekeza tafiti zaidijuu ya mofimu nyambulishi zote na mofimu nyingine zinazounda vitenzi vya Runyankore.