Ubadilishaji msimbo kwa walimu na athari zake kwa wanafunzi: mifano kutoka shule za sekondari za wilaya ya Kinondoni

dc.contributor.authorMtesigwa, Kapemba
dc.date.accessioned2021-08-11T11:51:12Z
dc.date.available2021-08-11T11:51:12Z
dc.date.issued2016
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.M7663)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ambao ulihusu Ubadilishaji Msimbo kwa walimu na Athari zake kwa wanafunzi ulikusudia kuchunguza kama kuna ubadilishaji msimbo katika shule za sekondari. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kubaini aina za ubadilishaji msimbo kati ya Kiswahili na kiingereza unaotumiwa na walimu wa shule za sekondari za wilaya ya Kinondoni, pili, kueleza sababu zinazo wafanya walimu wa shule za sekondari kubadilisha msimbo kati ya Kiswahili na kiingereza, na tatu, kujadili athari wanazozipata wanafunzi kutokana na walimu kubadilisha msimbo kati ya Kiswahili na kiingereza. Lengo la nne lilikuwa ni kutoa mapendekezo ya namna ya kupungaza ubadilishaji msimbo kati ya Kiswahili na kiingereza. Mtafiti alitumia mbinu za hojaji, ushuhudia jina usaili ilikupata data za kutosha za kukamilisha utafiti huu. Mtafiti alitumia watafiti wa walimu 15 na wanafunzi 108. Mkabala uliotumika kufafanua matokeo ya utafiti huu ni mkabala wakimaelezo na kiidadi. Nadharia ya Modeli ya Bell ya mwaka (1984) imetumika katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa walimu wanatumia aina mbili za ubadilishaji msimbo ambazo ni ubadilishaji msimbo ndani na ubadilishaji msimbo kati. Sababu inayowafanya walimu watumie ubadilishaji msimbo ni kuto kuimudu vema lugha ya kiingereza. Wanafunzi wanapata wakati mgumu kujibu mitihani yao kwa kiingereza. Kupunguza matumizi ya ubadilishaji msimbo, inapendekeza kuwa Kiswahili kitumike kufundishia katika shule za sekondari. Utafiti mwingine unaweza kuchunguza iwapo ubadilishaji msimbo nimatokeo ya kiwango duni cha umilisiwa lugha zinazo husishwa katika ubadilishaji msimbo.en_US
dc.identifier.citationMtesigwa, Kapemba (2016) Ubadilishaji msimbo kwa walimu na athari zake kwa wanafunzi: mifano kutoka shule za sekondari za wilaya ya Kinondoni, Master dissertation, University of Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15377
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectEnglish languageen_US
dc.subjectlanguage mixed,en_US
dc.subjectSecondary schoolsen_US
dc.subjectTeachersen_US
dc.subjectStudentsen_US
dc.subjectKinondoni districten_US
dc.titleUbadilishaji msimbo kwa walimu na athari zake kwa wanafunzi: mifano kutoka shule za sekondari za wilaya ya Kinondonien_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Kapemba Mtesigwa.pdf
Size:
7 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: