Ubadilishaji msimbo kwa walimu na athari zake kwa wanafunzi: mifano kutoka shule za sekondari za wilaya ya Kinondoni

Date

2016

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu ambao ulihusu Ubadilishaji Msimbo kwa walimu na Athari zake kwa wanafunzi ulikusudia kuchunguza kama kuna ubadilishaji msimbo katika shule za sekondari. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kubaini aina za ubadilishaji msimbo kati ya Kiswahili na kiingereza unaotumiwa na walimu wa shule za sekondari za wilaya ya Kinondoni, pili, kueleza sababu zinazo wafanya walimu wa shule za sekondari kubadilisha msimbo kati ya Kiswahili na kiingereza, na tatu, kujadili athari wanazozipata wanafunzi kutokana na walimu kubadilisha msimbo kati ya Kiswahili na kiingereza. Lengo la nne lilikuwa ni kutoa mapendekezo ya namna ya kupungaza ubadilishaji msimbo kati ya Kiswahili na kiingereza. Mtafiti alitumia mbinu za hojaji, ushuhudia jina usaili ilikupata data za kutosha za kukamilisha utafiti huu. Mtafiti alitumia watafiti wa walimu 15 na wanafunzi 108. Mkabala uliotumika kufafanua matokeo ya utafiti huu ni mkabala wakimaelezo na kiidadi. Nadharia ya Modeli ya Bell ya mwaka (1984) imetumika katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa walimu wanatumia aina mbili za ubadilishaji msimbo ambazo ni ubadilishaji msimbo ndani na ubadilishaji msimbo kati. Sababu inayowafanya walimu watumie ubadilishaji msimbo ni kuto kuimudu vema lugha ya kiingereza. Wanafunzi wanapata wakati mgumu kujibu mitihani yao kwa kiingereza. Kupunguza matumizi ya ubadilishaji msimbo, inapendekeza kuwa Kiswahili kitumike kufundishia katika shule za sekondari. Utafiti mwingine unaweza kuchunguza iwapo ubadilishaji msimbo nimatokeo ya kiwango duni cha umilisiwa lugha zinazo husishwa katika ubadilishaji msimbo.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.M7663)

Keywords

Swahili language, English language, language mixed,, Secondary schools, Teachers, Students, Kinondoni district

Citation

Mtesigwa, Kapemba (2016) Ubadilishaji msimbo kwa walimu na athari zake kwa wanafunzi: mifano kutoka shule za sekondari za wilaya ya Kinondoni, Master dissertation, University of Dar es Salaam