Nafasi ya lugha ya kiswahili katika mandhari- lugha ya jiji la Mbeya nchini Tanzania

dc.contributor.authorKawonga, Gervas
dc.date.accessioned2021-08-19T08:01:51Z
dc.date.available2021-08-19T08:01:51Z
dc.date.issued2020
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8701T34K396)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulihusu nafasi ya lugha ya Kiswahili katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Lengo kuu lilikuwa kuchunguza nafasi ya lugha ya Kiswahili katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Malengo mahususi yalikuwa matatu: kwanza, kubainisha ruwaza za lugha kwenye mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Pili, kudhihirisha nafasi ya lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia ruwaza za lugha kwenye mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Tatu, kuwianisha sera ya lugha ya Tanzania na nafasi ya lugha kwenye mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ubeberu wa Kiisimu yenye msingi kwamba katika jamii kuna vipengele vya kimfumo na kiitikadi vinavyosababisha uhusiano usio wa usawa miongoni mwa lugha za jamii mbalimbali. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya upigaji wa picha za mabango ya makampuni ya mawasiliano ya simu na mbinu ya usaili. Uchambuzi wa data za mabango ya makampuni ya mawasiliano ya simu ulifanyika kwa mbinu ya usomaji wa matini na Programu Tarakilishi ya Takwimu (PTT). Uwasilishaji wa data umefanyika kwa kutumia vielelezo vya majedwali, grafu na picha kwa data za kiidadi za mabango ya makampuni ya mawasiliano ya simu. Nukuu za usaili na ufafanuzi wa kinathari umetumika kwa data za kitaamuli. Matokeo yanaonesha kwamba kuna ruwaza nne za lugha katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Ruwaza zilizobainishwa ni Kiswahili pekee, Kiingereza pekee, Kiswahili-Kiingereza na Kiingereza-Kiswahili. Kiswahili kinajitokeza kwa asilimia 54.5 katika ruwaza ya Kiswahili pekee mbele ya Kiingereza. Kwa kigezo cha ukubwa wa maandishi Kiswahili kinajitokeza cha kwanza kwa asilimia 63 kwa maandishi makubwa zaidi kuliko Kiingereza. Vilevile, kwa kigezo cha idadi ya maneno Kiswahili kinajitokeza katika nafasi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 72.23. Kwa hiyo, Kiswahili kinajitokeza katika nafasi ya kwanza kimatumizi katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Aidha, kuna uwiano baina ya Sera ya Lugha ya Tanzania na nafasi ya matumizi ya lugha katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya. Hata hivyo, tunapendekeza serikali ifanye mapitio ya sera ya lugha ili kuunda kanuni za matumizi ya lugha katika mandhari-lugha na kuweka urari wa matumizi ya lugha katika mandhari-lugha. Vilevile, tafiti fuatishi zifanyike kwa kuchunguza mabango ya makampuni mahususi tofautitofauti ili kupanua uelewa kuhusu ruwaza za lugha, nafasi ya Kiswahili na uwiano wa nafasi ya matumizi ya lugha na Sera ya lugha ya Tanzania.en_US
dc.identifier.citationKawonga, G (2020) Nafasi ya lugha ya kiswahili katika mandhari- lugha ya jiji la Mbeya nchini Tanzania, Doctoral dissertation , University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15432
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es salaamen_US
dc.subjectBantu languagesen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectMbeya Municipalen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleNafasi ya lugha ya kiswahili katika mandhari- lugha ya jiji la Mbeya nchini Tanzaniaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Gervas Kawonga.pdf
Size:
363.07 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections