Viangami katika Kipemba

dc.contributor.authorSaid, Daulat Abdalla
dc.date.accessioned2019-07-06T09:32:36Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:38Z
dc.date.available2019-07-06T09:32:36Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:38Z
dc.date.issued2011
dc.descriptionAvailable in printen_US
dc.description.abstractUtafiti huu unaohusu viangami katika Kipemba umegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi ambao unajumuisha vipengele vya awali vya utafiti. Vipengele vilivyoelezwa ni usuli wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti na mawanda na mipaka ya utafiti. Sura ya pili, inaeleza mapitio ya machapisho na kiunzi cha kinadharia, ambapo imetumika nadharia ya Zwicky (1977) kama ilivyofafanuliwa na Katamba na Stonham (2006). Aidha, sura ya tatu inajadili mbinu na njia za utafiti. Hapa kuna vipengele kama eneo la utafiti, usampulishaji, watoa taarifa, vifaa vya utafiti, ukusanyaji wa data, vyanzo vya data, mbinu za uchambuzi wa data na uwasilishaji wa data. Sura ya nne, inaeleza vipengele vinavyohusiana na uchambuzi wa data. Vipengele hivyo vimegawanywa katika sehemu nne kubwa. Sehemu ya kwanza ni aina za viangami zilizomo katika Kipemba. Aina iliyoelezwa ni viangami sahili; viangami awali na viangami tamati. Sehemu ya pili ni mofimu ambazo ni viangami katika Kipemba ambapo kuna viangami vinavyotokana na udondoshaji, viangami vya mofimu maalumu zenye maana ya kileksika na viangami viwili katika kiegemewa kimoja. Sehemu ya tatu ni kategoria za maneno ambazo ni viegemewa vya viangami katika Kipemba; nazo ni nomino, viwakilishi, vivumishi, vielezi, viunganishi na viingizi na sehemu ya nne ni maelezo elekezi kuhusu uchambuzi wa viangami. Sura ya tano, inatoa muhtasari wa jumla wa matokeo ya utafiti, hitimisho na mapendekezo kwa ajili ya tafiti fuatishi.en_US
dc.identifier.citationSaid, D. A (2011) Viangami katika Kipemba.Tasinifu ya M.A. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Inapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspxen_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3419
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectPemba languageen_US
dc.subjectPemba Islanden_US
dc.titleViangami katika Kipembaen_US
dc.typeThesisen_US

Files