Viangami katika Kipemba
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu unaohusu viangami katika Kipemba umegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi ambao unajumuisha vipengele vya awali vya utafiti. Vipengele vilivyoelezwa ni usuli wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti na mawanda na mipaka ya utafiti. Sura ya pili, inaeleza mapitio ya machapisho na kiunzi cha kinadharia, ambapo imetumika nadharia ya Zwicky (1977) kama ilivyofafanuliwa na Katamba na Stonham (2006). Aidha, sura ya tatu inajadili mbinu na njia za utafiti. Hapa kuna vipengele kama eneo la utafiti, usampulishaji, watoa taarifa, vifaa vya utafiti, ukusanyaji wa data, vyanzo vya data, mbinu za uchambuzi wa data na uwasilishaji wa data. Sura ya nne, inaeleza vipengele vinavyohusiana na uchambuzi wa data. Vipengele hivyo vimegawanywa katika sehemu nne kubwa. Sehemu ya kwanza ni aina za viangami zilizomo katika Kipemba. Aina iliyoelezwa ni viangami sahili; viangami awali na viangami tamati. Sehemu ya pili ni mofimu ambazo ni viangami katika Kipemba ambapo kuna viangami vinavyotokana na udondoshaji, viangami vya mofimu maalumu zenye maana ya kileksika na viangami viwili katika kiegemewa kimoja. Sehemu ya tatu ni kategoria za maneno ambazo ni viegemewa vya viangami katika Kipemba; nazo ni nomino, viwakilishi, vivumishi, vielezi, viunganishi na viingizi na sehemu ya nne ni maelezo elekezi kuhusu uchambuzi wa viangami. Sura ya tano, inatoa muhtasari wa jumla wa matokeo ya utafiti, hitimisho na mapendekezo kwa ajili ya tafiti fuatishi.