Usawiri wa mhusika mtoto wa kike katika ngano za kingoni

dc.contributor.authorMaharani, Hadija S
dc.date.accessioned2021-02-15T06:38:52Z
dc.date.available2021-02-15T06:38:52Z
dc.date.issued2018
dc.descriptionAvailable in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8704.T34M335)en_US
dc.description.abstractTasnifu hii ni zao la utafiti kuhusu usawiri wa mhusika mtoto wa kike katika ngano za Kingoni. Tasnifu imechunguza namna mhusika mtoto wa kike anavyosawiriwa katika ngano za Kingoni kupitia sifa zinazombainisha mhusika huyo pamoja na dhima za usawiri wake. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka uwandani, na mbinu zilizotumika kukusanyia data hizo ni mbinu ya usikilizaji wa simulizi za ngano na mbinu ya mahojiano. Nadharia ya Uhalisia imemwongoza mtafiti katika uchambuzi wa ngano tano zilizoteuliwa. Uchambuzi wa ngano hizo umebainisha kwamba, mhusika mtoto wa kike katika ngano za Kingoni amesawiriwa kuwa ni kuimbe mwenye mapenzi ya dhati, mkaidi kwa wazazi wake, chanzo cha matatizo, mzinifu, mwongo, na mtumishi wa kazi za nyumbani. Kwa upande mwingine, imegunduliwa kuwa usawiri wa mhusika mtoto wa kike katika ngano za Kingoni zilizochunguzwa, unabeba dhima ya kuibua dhamira, kubainisha migogoro na masuluhisho yake, kuibua hisia kwa hadhira, kubainisha falsafa ya jamii, kuwatambulisha wahusika wengine, kuleta usikivu kwa hadhira kwa kuijengea taharuki pamoja na kutoa mafunzo katika jamii husika. Kwa kumalizia, utafiti umetoa hitimisho la jumla la tasnifu nzima na kupendekeza maeneo mengine ambayo yanahitaji kufanyiwa utafiti zaidi.en_US
dc.identifier.citationMaharani, Hadija S (2018) Usawiri wa mhusika mtoto wa kike katika ngano za kingoni ,Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/14810
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectNgoni (African people)en_US
dc.subjectHistoryen_US
dc.subjectRitualsen_US
dc.subjectcustom and manneren_US
dc.subjectGirlsen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleUsawiri wa mhusika mtoto wa kike katika ngano za kingonien_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Hadija Shaweji Maharani.pdf
Size:
177.08 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: