Usawiri wa mhusika mtoto wa kike katika ngano za kingoni

Date

2018

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Tasnifu hii ni zao la utafiti kuhusu usawiri wa mhusika mtoto wa kike katika ngano za Kingoni. Tasnifu imechunguza namna mhusika mtoto wa kike anavyosawiriwa katika ngano za Kingoni kupitia sifa zinazombainisha mhusika huyo pamoja na dhima za usawiri wake. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka uwandani, na mbinu zilizotumika kukusanyia data hizo ni mbinu ya usikilizaji wa simulizi za ngano na mbinu ya mahojiano. Nadharia ya Uhalisia imemwongoza mtafiti katika uchambuzi wa ngano tano zilizoteuliwa. Uchambuzi wa ngano hizo umebainisha kwamba, mhusika mtoto wa kike katika ngano za Kingoni amesawiriwa kuwa ni kuimbe mwenye mapenzi ya dhati, mkaidi kwa wazazi wake, chanzo cha matatizo, mzinifu, mwongo, na mtumishi wa kazi za nyumbani. Kwa upande mwingine, imegunduliwa kuwa usawiri wa mhusika mtoto wa kike katika ngano za Kingoni zilizochunguzwa, unabeba dhima ya kuibua dhamira, kubainisha migogoro na masuluhisho yake, kuibua hisia kwa hadhira, kubainisha falsafa ya jamii, kuwatambulisha wahusika wengine, kuleta usikivu kwa hadhira kwa kuijengea taharuki pamoja na kutoa mafunzo katika jamii husika. Kwa kumalizia, utafiti umetoa hitimisho la jumla la tasnifu nzima na kupendekeza maeneo mengine ambayo yanahitaji kufanyiwa utafiti zaidi.

Description

Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8704.T34M335)

Keywords

Swahili literature, Ngoni (African people), History, Rituals, custom and manner, Girls, Tanzania

Citation

Maharani, Hadija S (2018) Usawiri wa mhusika mtoto wa kike katika ngano za kingoni ,Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam