Dhima ya mhusika mlevi na muakiso wa uhalisi wa kauli zake: mifano kutoka lina ubani na mabepari wa bongo

dc.contributor.authorMlelwa, Lazaro
dc.date.accessioned2019-07-31T14:51:47Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:39Z
dc.date.available2019-07-31T14:51:47Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:39Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionAvailable in print formen_US
dc.description.abstractUtafiti huu umejadili kuhusu Mhusika mlevi na uhalisi wa kauli na matendo yake katika fasihi andishi ya Kiswahili, kwa kutumia mifano kutoka Lina Ubani na Mabepari wa Bongo. Tatizo lililojenga utafiti ni kutokana na muonekano wa mlevi wa kila siku katika jamii, na matumizi ya mhusika mlevi katika kazi za fasihi. Mlevi siku zote huonekana kama punguani, mtu dhalili, na msema ovyo, mtu aliyejishindwa na anayeshindwa kuzuia hisia zake pindi anapolewa. Swali tunalojiuliza ni kwa nini watunzi wa fasihi wanamtumia katika katika kazi zao ili hali wanajua hali yake? Dhima yake halisi ni ipi katika jamii husika? Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani, ambapo matini nyingi zilisomwa ili kupata ruwaza ya jumla kuhusu mhusika mlevi na uhalisi wa kauli na matendo yake katika fasihi andishi. Utafiti huu umeongozwa na nadharia mbili, nadharia ya Ucheshi na nadharia ya saikochanganuzi. Utafiti umebaini kuwa kuna uhalisi fulani katika baadhi ya matendo na kauli za mhusika mlevi. Ingawa mlevi mara nyingi hasikilizwi, lakini ni mtu anayeeleza yale ambayo mhusika mwingine wa kawaida hawezi kuyaeleza. Hii ni kwa sababu watu wengi humuona mlevi kama mtu aliyepoteza urazini na hivyo huongea tu kama mwendawazimu, kwa minajili hiyo wengi wanampuuza lakini kwa hakika ni mtu anayeakisi uhalisi wa jamii yake bila woga. Utafiti huu umependekeza kuwa, ijapokuwa mlevi huonekana kama mwendawazimu, hata hivyo anapaswa kusikilizwa na asipuuzwe asilani. Mwisho utafiti umependekeza maeneo mengine yanayostahili kufanyiwa utafiti zaidi: matumizi ya mhusika mlevi yatafitiwe katika riwaya, ushairi na fasihi simulizi ili kubaini dhima yake katika fasihi.en_US
dc.identifier.citationMlelwa, L. (2012). Dhima ya mhusika mlevi na muakiso wa uhalisi wa kauli zake: mifano kutoka lina ubani na mabepari wa bongo. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at (http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/search.aspx)en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3438
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectLina ubanien_US
dc.subjectMabepari wa bongoen_US
dc.titleDhima ya mhusika mlevi na muakiso wa uhalisi wa kauli zake: mifano kutoka lina ubani na mabepari wa bongoen_US
dc.typeThesisen_US

Files