Sihiri katika tamthilia ya Kiswahili: uchunguzi wa kazi za Emmanuel Mbogo, Ngoma ya Ng’wanamalundi (2008) na Sundiata (2011)

dc.contributor.authorKayombo, Restuta Thadei
dc.date.accessioned2021-09-28T06:41:17Z
dc.date.available2021-09-28T06:41:17Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8703.5.K3965)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu, Sihiri katika Tamthilia ya Kiswahili: Uchunguzi wa Kazi za Emmanuel Mbogo, Ngoma ya N’wanamalundi (2008) na Sundiata (2011). Tumefanya utafiti ili kubaini kama kuna matumizi ya sihiri katika kazi teule za tamthilia au la. Jambo hili lilitokana na mvutano ulioibuka baina ya wachambuzi na wabobezi katika fasihi ya Kiswahili, hususan tamthilia ya Kiswahili kutokana na kuwepo au kutokuwepo kwa matumizi hayo huku mtafiti akilenga vipengele viwili tu ambavyo ni uchawi na uganga. Mvutano huo unawahusisha wale wanaodai kuwa kuna matumizi makubwa ya sihiri katika ya Ngoma limemvutia sana mtafiti kiasi cha kuamua kulichunguza jambo hili kwa kutalii tamthilia nyingine kutoka kwa mtunzi huyohuyo ambayo ni Sundiata (2011). Katika kutafuta ukweli wa madai haya, utafiti huu umechunguza matumizi ya sihiri kupitia uchawi na uganga katika matini teule. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kubainisha matumizi ya sihiri yalivyojitokeza katika tamthilia zilizoandikwa na Mbogo Ngoma ya Ng’wanamalundi (2008) na Sundiata 2011, kufafFanua sababu za matumizi ya sihiri kwa wahusika wanaoziumba tamthilia teule. Nadharia iliyotumika katika uchambuzi wa data ni nadharia ya Uhalisiamazingaombwe iliyoasisiwa na Franz Roh (1920). Utafiti huu ni wa maktabani. Ili kufikia malengo ya utafiti huu, mbinu ya usomaji makini wa matini ilitumika katika kukusanya data kwa kutumia maktaba za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Data zilizokusanywa zimewasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti umebaini kwamba, tamthilia teule zimesheheni matumizi ya sihiri kupitia uchawi na uganga ambapo mtafiti amebaini sababu mbalimbali za mtunzi kutumia dhana hizo. Pia mtafiti amebaini athari mbalimbali zinazotokana na matunizi hayo kupitia wahusika wa tamthilia hizo ambazo zimechangia katika maendeleo ya uandishi wa tamthilia ya Kiswahili.en_US
dc.identifier.citationKayombo, R.T (2019). Sihiri katika tamthilia ya Kiswahili: uchunguzi wa kazi za Emmanuel Mbogo, Ngoma ya Ng’wanamalundi (2008) na Sundiata (2011), (M.A Kiswahili). University of Dar es Salaam. Dar es Salaam)en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15627
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectSwahili dramaen_US
dc.subjectMagic in Literatureen_US
dc.subjectEmmanuel Mbogoen_US
dc.titleSihiri katika tamthilia ya Kiswahili: uchunguzi wa kazi za Emmanuel Mbogo, Ngoma ya Ng’wanamalundi (2008) na Sundiata (2011)en_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Restuta Thadei Kayombo.pdf
Size:
189.69 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: