Sihiri katika tamthilia ya Kiswahili: uchunguzi wa kazi za Emmanuel Mbogo, Ngoma ya Ng’wanamalundi (2008) na Sundiata (2011)

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu, Sihiri katika Tamthilia ya Kiswahili: Uchunguzi wa Kazi za Emmanuel Mbogo, Ngoma ya N’wanamalundi (2008) na Sundiata (2011). Tumefanya utafiti ili kubaini kama kuna matumizi ya sihiri katika kazi teule za tamthilia au la. Jambo hili lilitokana na mvutano ulioibuka baina ya wachambuzi na wabobezi katika fasihi ya Kiswahili, hususan tamthilia ya Kiswahili kutokana na kuwepo au kutokuwepo kwa matumizi hayo huku mtafiti akilenga vipengele viwili tu ambavyo ni uchawi na uganga. Mvutano huo unawahusisha wale wanaodai kuwa kuna matumizi makubwa ya sihiri katika ya Ngoma limemvutia sana mtafiti kiasi cha kuamua kulichunguza jambo hili kwa kutalii tamthilia nyingine kutoka kwa mtunzi huyohuyo ambayo ni Sundiata (2011). Katika kutafuta ukweli wa madai haya, utafiti huu umechunguza matumizi ya sihiri kupitia uchawi na uganga katika matini teule. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kubainisha matumizi ya sihiri yalivyojitokeza katika tamthilia zilizoandikwa na Mbogo Ngoma ya Ng’wanamalundi (2008) na Sundiata 2011, kufafFanua sababu za matumizi ya sihiri kwa wahusika wanaoziumba tamthilia teule. Nadharia iliyotumika katika uchambuzi wa data ni nadharia ya Uhalisiamazingaombwe iliyoasisiwa na Franz Roh (1920). Utafiti huu ni wa maktabani. Ili kufikia malengo ya utafiti huu, mbinu ya usomaji makini wa matini ilitumika katika kukusanya data kwa kutumia maktaba za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Data zilizokusanywa zimewasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti umebaini kwamba, tamthilia teule zimesheheni matumizi ya sihiri kupitia uchawi na uganga ambapo mtafiti amebaini sababu mbalimbali za mtunzi kutumia dhana hizo. Pia mtafiti amebaini athari mbalimbali zinazotokana na matunizi hayo kupitia wahusika wa tamthilia hizo ambazo zimechangia katika maendeleo ya uandishi wa tamthilia ya Kiswahili.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8703.5.K3965)
Keywords
Swahili literature, Swahili drama, Magic in Literature, Emmanuel Mbogo
Citation
Kayombo, R.T (2019). Sihiri katika tamthilia ya Kiswahili: uchunguzi wa kazi za Emmanuel Mbogo, Ngoma ya Ng’wanamalundi (2008) na Sundiata (2011), (M.A Kiswahili). University of Dar es Salaam. Dar es Salaam)