Mabadiliko ya maadili katika tamthiliya ya Kiswahili Tanzania

dc.contributor.authorLusasi, Zaveria Edward
dc.date.accessioned2020-04-07T14:49:39Z
dc.date.available2020-04-07T14:49:39Z
dc.date.issued2017
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8702.L87)en_US
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza mabadiliko ya maadili katika tamthiliya ya Kiswahili inayochezwa katika runinga nchini Tanzania, mifano kutoka katika tamthiliya ya Siri ya Mtungi. Data za uwandani zilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu za ukusanyaji wa data. Mbinu hizo ni majadiliano ya vikundi, mahojiano na hojaji. Nadharia ya Uhistoria Mpya ilitumika katika kufanikisha na kufikia malengo ya utafiti huu, hasa katika mchakato mzima wa uchambuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa ni kweli yapo maadili ya Kitanzania na yasiyo ya Kitanzania katika tamthiliya ya Kiswahili, hususani ndani ya tamthiliya ya Siri ya Mtungi. Aidha, sababu za mabadiliko hayo ya maadili katika jamii ya Watanzania zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya jamii yanayosababishwa na mambo makuu manne. Mambo hayo ni utandawazi, soko huria, uliberali mamboleo na mwingiliano wa jamii, ambapo kwa sababu ya uchumi duni wa jamii, Baadhi ya Watanzania wanajikuta ni watumwa wa kifikra na kimawazo wakifuata matakwa ya nchi za kibeberu inayofungashwa kupitia katika misaada, hisani na kwa jina la “uwekezaji kutoka nje”. Jambo hilo linachangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili katika jamii. Kwa hiyo, jamii ya Watanzania inapaswa kuutunza utamaduni wake wa asili kwa kuyalinda maadili ya jamii. Hii ni kwa sababu jamii haiwezi kuendelea kwa kuiga au kupokea maadili ya jamii nyingine. Hivyo basi, jamii ifanye kila jitihada kujiepusha na kutegemea misaada na hisani kutoka nje.en_US
dc.identifier.citationLusasi, Z.E. (2017) Mabadiliko ya maadili katika tamthiliya ya Kiswahili Tanzania. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/9166
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectSocial ethicsen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleMabadiliko ya maadili katika tamthiliya ya Kiswahili Tanzaniaen_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Zaveria Edward Lusasi.pdf
Size:
100.95 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: