Mabadiliko ya maadili katika tamthiliya ya Kiswahili Tanzania

Loading...
Thumbnail Image
Date
2017
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza mabadiliko ya maadili katika tamthiliya ya Kiswahili inayochezwa katika runinga nchini Tanzania, mifano kutoka katika tamthiliya ya Siri ya Mtungi. Data za uwandani zilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu za ukusanyaji wa data. Mbinu hizo ni majadiliano ya vikundi, mahojiano na hojaji. Nadharia ya Uhistoria Mpya ilitumika katika kufanikisha na kufikia malengo ya utafiti huu, hasa katika mchakato mzima wa uchambuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa ni kweli yapo maadili ya Kitanzania na yasiyo ya Kitanzania katika tamthiliya ya Kiswahili, hususani ndani ya tamthiliya ya Siri ya Mtungi. Aidha, sababu za mabadiliko hayo ya maadili katika jamii ya Watanzania zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya jamii yanayosababishwa na mambo makuu manne. Mambo hayo ni utandawazi, soko huria, uliberali mamboleo na mwingiliano wa jamii, ambapo kwa sababu ya uchumi duni wa jamii, Baadhi ya Watanzania wanajikuta ni watumwa wa kifikra na kimawazo wakifuata matakwa ya nchi za kibeberu inayofungashwa kupitia katika misaada, hisani na kwa jina la “uwekezaji kutoka nje”. Jambo hilo linachangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili katika jamii. Kwa hiyo, jamii ya Watanzania inapaswa kuutunza utamaduni wake wa asili kwa kuyalinda maadili ya jamii. Hii ni kwa sababu jamii haiwezi kuendelea kwa kuiga au kupokea maadili ya jamii nyingine. Hivyo basi, jamii ifanye kila jitihada kujiepusha na kutegemea misaada na hisani kutoka nje.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8702.L87)
Keywords
Swahili literature, Social ethics, Tanzania
Citation
Lusasi, Z.E. (2017) Mabadiliko ya maadili katika tamthiliya ya Kiswahili Tanzania. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.