library@udsm.ac.tz +255753225900
Emblem
Univerisity of Dar es Salaam

Library Repository

Books

Matumizi ya lugha yanavyo ibua dhamira za kisiasa katika diwani za fungate ya uhuru (1988) na wasakatonge (2003)

dc.contributor.authorKasege, Upendo
dc.date.accessioned2021-08-11T12:38:28Z
dc.date.available2021-08-11T12:38:28Z
dc.date.issued2013
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.K373)en_US
dc.description.abstractUtafitihuuunahusu “Matumizi ya Lugha yanavyoibua Dhamira za kisasa katika diwani za fungate ya uhuru na Wasakatonge.” Utafiti huu unachambua namna matumizi ya lugha yanavyo jitokeza na yanavyoweza kupatiwa maana kulingana na hali, historia, na mazingira ya msomaji. Malengo ya utafiti huu ni kuchambua kwa kina matumizi ya lugha katika diwani teule, na kueleza jinsi matumizi hayo ya lugha yanavyoibua dhamira za kisiasa katika diwani hizo pamoja na mtazamo wa mwandishi kuhusu masuala hayo ya kisiasa. Katika utafiti huu mbinu za utafiti wa maktabani, na utafiti mdogo wa uwandani, zimetumika. Mtafiti ameweza kusoma, kudurusu vitabu, majarida, nanyaraka mbalimbali katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na makava ziilikupata data za utafiti huu. Pia mahojiano kati ya mtafiti na mwandishi (M.S. Khatib) yalifanyika ilikujua maisha yake kwa ujumla na kazi zake za sanaa. Utafiti huu umefanywa kwa kutumia nadharia ya Semiotiki kwa kuzingatia aina tano za ishara zilizopendekezwa na Barthes. Lugha katika diwani mbili za fungate ya Uhuru na Wasakatonge imechambuliwa kwa kina na kuonesha jinsi ilivyosaidia kuibua dhamira za kisiasa. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba kazi ya fasihi ina urejerezi wanje. Ishara husika hupatiwa maana na kuibua dhamira za kisiasa kulingana na uzoevu, historia, utamaduni, na mtazamo wamsomaji. Kwa kutumia lugha ya kisanaa, mwandishi ameweza kuibua dhamira mbalimbali za kisiasa. Miongoni mwa dhamira zilizojitokeza ni pamoja na umaskini, matumizi mabaya ya mali ya umma, uchu wa madaraka, matabaka, na kukosekana kwahaki. Pia matokeo ya utafiti huu yame baini kwamba kwa kiasi kikubwa mwandishi ametumia mbinu za kisanaa, hususani katika matumizi ya lugha, ili kufikisha ujumbe kwa hadhira lengwa. Mbinu hizo ni pamoja na tamathali za semi, takiriri, nidaa, ishara, taswira, lugha ya majigambo, na misemo. Vile vile, matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba uelewekaji waushairi wa M.S. Khatibu nategemea umahiri wa wasomaji wake katika kufumbua taswira na ishara mbalimbali zilizojengwa kupitia lugha iliyotumka.en_US
dc.identifier.citationKasege, Upendo (2013) Matumizi ya lugha yanavyo ibua dhamira za kisiasa katika diwani za fungate ya uhuru (1988) na wasakatonge (2003), Master dissertation, University of Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15378
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectHistory and criticismen_US
dc.subjectDiwani za fungate (1988 ) na wasakatonge ( 2003 )en_US
dc.subjectSwahili poetryen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectPoetryen_US
dc.titleMatumizi ya lugha yanavyo ibua dhamira za kisiasa katika diwani za fungate ya uhuru (1988) na wasakatonge (2003)en_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Kasege Upendo.pdf
Size:
102.26 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: