Matumizi ya lugha yanavyo ibua dhamira za kisiasa katika diwani za fungate ya uhuru (1988) na wasakatonge (2003)
Loading...
Date
2013
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafitihuuunahusu “Matumizi ya Lugha yanavyoibua Dhamira za kisasa katika diwani za fungate ya uhuru na Wasakatonge.” Utafiti huu unachambua namna matumizi ya lugha yanavyo jitokeza na yanavyoweza kupatiwa maana kulingana na hali, historia, na mazingira ya msomaji. Malengo ya utafiti huu ni kuchambua kwa kina matumizi ya lugha katika diwani teule, na kueleza jinsi matumizi hayo ya lugha yanavyoibua dhamira za kisiasa katika diwani hizo pamoja na mtazamo wa mwandishi kuhusu masuala hayo ya kisiasa. Katika utafiti huu mbinu za utafiti wa maktabani, na utafiti mdogo wa uwandani, zimetumika. Mtafiti ameweza kusoma, kudurusu vitabu, majarida, nanyaraka mbalimbali katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na makava ziilikupata data za utafiti huu. Pia mahojiano kati ya mtafiti na mwandishi (M.S. Khatib) yalifanyika ilikujua maisha yake kwa ujumla na kazi zake za sanaa. Utafiti huu umefanywa kwa kutumia nadharia ya Semiotiki kwa kuzingatia aina tano za ishara zilizopendekezwa na Barthes. Lugha katika diwani mbili za fungate ya Uhuru na Wasakatonge imechambuliwa kwa kina na kuonesha jinsi ilivyosaidia kuibua dhamira za kisiasa. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba kazi ya fasihi ina urejerezi wanje. Ishara husika hupatiwa maana na kuibua dhamira za kisiasa kulingana na uzoevu, historia, utamaduni, na mtazamo wamsomaji. Kwa kutumia lugha ya kisanaa, mwandishi ameweza kuibua dhamira mbalimbali za kisiasa. Miongoni mwa dhamira zilizojitokeza ni pamoja na umaskini, matumizi mabaya ya mali ya umma, uchu wa madaraka, matabaka, na kukosekana kwahaki. Pia matokeo ya utafiti huu yame baini kwamba kwa kiasi kikubwa mwandishi ametumia mbinu za kisanaa, hususani katika matumizi ya lugha, ili kufikisha ujumbe kwa hadhira lengwa. Mbinu hizo ni pamoja na tamathali za semi, takiriri, nidaa, ishara, taswira, lugha ya majigambo, na misemo. Vile vile, matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba uelewekaji waushairi wa M.S. Khatibu nategemea umahiri wa wasomaji wake katika kufumbua taswira na ishara mbalimbali zilizojengwa kupitia lugha iliyotumka.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.K373)
Keywords
History and criticism, Diwani za fungate (1988 ) na wasakatonge ( 2003 ), Swahili poetry, Swahili literature, Poetry
Citation
Kasege, Upendo (2013) Matumizi ya lugha yanavyo ibua dhamira za kisiasa katika diwani za fungate ya uhuru (1988) na wasakatonge (2003), Master dissertation, University of Dar es Salaam