Utohozi wa nomino za kiswahili na athari yake katika ngeli za kihaya

dc.contributor.authorAdolph, Editha
dc.date.accessioned2019-11-06T14:49:46Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:35Z
dc.date.available2019-11-06T14:49:46Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:35Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8834A36)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umechunguza utohozi wa nomino za Kiswahili katika Kihaya na athari yake katika ngeli za Kihaya. Utafiti umefanyika katika kata za Izigo, Mayondwe na Muhutwe wilayani Muleba mkoa wa Kagera nchini Tanzania. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika ya Kiparsky (1982). Aidha, data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji, mahojiano, ushuhudiaji pamoja na njia za uwandani na maktabani. Halikadhalika, mkabala usio wa kiidadi ulitumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa lugha ya Kihaya imekopa baadhi ya nomino kutoka katika Kiswahili. Baada ya nomino za Kiswahili kutoholewa katika Kihaya, zimefanyiwa michakato ya kifonolojia na kimofolojia kadiri ya kanuni na taratibu za lugha ya Kihaya ili ziweze kukubalika katika lugha ya Kihaya. Vilevile utafiti huu umebaini kuwa kuna athari ya kingeli inayotokana na utohozi wa nomino za Kiswahili katika lugha ya Kihaya. Kwa mfano, athari ya nomino za asili za Kihaya kubadili ngeli zake. Aidha, katika utafiti huu inapendekezwa kwamba uchunguzi ufanyike kuhusu mabadiliko ya ngeli yaliyotokea kuanzia zama za Mame-Bantu. Pia, mtafiti anapendekeza maeneo mengine yafanyiwe tafiti, mfano, uainishaji wa lahaja za Kihaya, fonolojia, semantiki, sintaksia na mofolojia ya Kihaya. Aidha, kuna haja ya kufanya uchunguzi tena kuhusu utohozi wa nomino za Kiswahili katika Kihaya kwa miaka ijayo kwani ni wazi kuwa mchakato wa ukopaji na utohozi ni endelevu.en_US
dc.identifier.citationAdolph, E. (2014) Utohozi wa nomino za kiswahili na athari yake katika ngeli za kihaya, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3385
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectHaya languageen_US
dc.subjectNounsen_US
dc.subjectNominalsen_US
dc.titleUtohozi wa nomino za kiswahili na athari yake katika ngeli za kihayaen_US
dc.typeThesisen_US
Files