Utohozi wa nomino za kiswahili na athari yake katika ngeli za kihaya

No Thumbnail Available
Date
2014
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza utohozi wa nomino za Kiswahili katika Kihaya na athari yake katika ngeli za Kihaya. Utafiti umefanyika katika kata za Izigo, Mayondwe na Muhutwe wilayani Muleba mkoa wa Kagera nchini Tanzania. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika ya Kiparsky (1982). Aidha, data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji, mahojiano, ushuhudiaji pamoja na njia za uwandani na maktabani. Halikadhalika, mkabala usio wa kiidadi ulitumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa lugha ya Kihaya imekopa baadhi ya nomino kutoka katika Kiswahili. Baada ya nomino za Kiswahili kutoholewa katika Kihaya, zimefanyiwa michakato ya kifonolojia na kimofolojia kadiri ya kanuni na taratibu za lugha ya Kihaya ili ziweze kukubalika katika lugha ya Kihaya. Vilevile utafiti huu umebaini kuwa kuna athari ya kingeli inayotokana na utohozi wa nomino za Kiswahili katika lugha ya Kihaya. Kwa mfano, athari ya nomino za asili za Kihaya kubadili ngeli zake. Aidha, katika utafiti huu inapendekezwa kwamba uchunguzi ufanyike kuhusu mabadiliko ya ngeli yaliyotokea kuanzia zama za Mame-Bantu. Pia, mtafiti anapendekeza maeneo mengine yafanyiwe tafiti, mfano, uainishaji wa lahaja za Kihaya, fonolojia, semantiki, sintaksia na mofolojia ya Kihaya. Aidha, kuna haja ya kufanya uchunguzi tena kuhusu utohozi wa nomino za Kiswahili katika Kihaya kwa miaka ijayo kwani ni wazi kuwa mchakato wa ukopaji na utohozi ni endelevu.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8834A36)
Keywords
Haya language, Nouns, Nominals
Citation
Adolph, E. (2014) Utohozi wa nomino za kiswahili na athari yake katika ngeli za kihaya, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.