Mchomozo wa kipragmatiki katika nagona na mzingile: uchunguzi wa ‘kimya’

dc.contributor.authorDzomba, Edwell
dc.date.accessioned2020-12-04T12:10:29Z
dc.date.available2020-12-04T12:10:29Z
dc.date.issued2018
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.Z5.T34D964 )en_US
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza kimya kama mchomozo wa kipragmatiki katika riwaya mbili za Euphrase Kezilahabi ambazo ni Nagona na Mzingile. Mtafiti alikusanya data kwa kutumia mbinu ya usomaji matini. Sehemu zote zilizoandikwa neon ‘kimya’ na taarifa zinazozunguka neon hilo zilikusanywa kama data za kufanyia utafiti katika mazungumzo ya wahusika. Kila kimya kilipewa alama na kasha kikachambuliwa kwa kutumia mkabala wa kielimu-mitindo. Data zilichambuliwa kwa kutumia Mkabala wa kielimu-mtindo na Mkabala wa Korasi katika fasihi ambapo misingi ya Nadharia ya Uhusisho ya Sperber na Wilson (1986, 1995) na Nadharia ya Korasi katika Fasihi ya Mutembei (2012) imeunganishwa kuchunguza data. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, kimya katika riwaya za Kiswahili ni jambo la msingi na linahitaji umakini katika kuchunguza fani na maudhui ya riwaya za Kiswahili. Aidha, utafiti huu uligundua kuwa elimu-mtindo ni njia ya kipekee inayoweza kubainisha mtindo wa mwandishi kwa kina. Kupitia Mkabala wa Elimu-mitindo, kazi hii iliweza kuibua mtindo wa Kezilahabi katika matumizi ya kimya kuwasilisha mawazo yake. Kwa kuwa, kimya kinawasilisha mawazo yake. Kwa kuwa, kimya kinawasilisha maana iliyofichika na isiyo ya moja kwa moja, mkabala wa kielimu-mtindo umetumika kuchunguza mtindo wa Kezilahabi wa kumtaka msomaji aingilie kazi kwa undani kupitia matumizi ya kimya. Mkabala huu umeoneshwa na kufafanuaa maana zinazowasilishwa katika kimya hicho. Kwa hiyo, kuna haja ya kuchunguza kimya katika riwaya zingine za Kiswahili kwa kutumia mkabala na nadharia za kielimu-mitindo ili kuweza kubaini namna waandishi wanavyokitumia kuwasilisha maudhui yao katika mitindo mbalimbali.en_US
dc.identifier.citationDzomba, E. (2018) Mchomozo wa kipragmatiki katika nagona na mzingile: uchunguzi wa ‘kimya’, Master dissertation, University of Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/13639
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectLanguage and languagesen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectFolk literratureen_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.titleMchomozo wa kipragmatiki katika nagona na mzingile: uchunguzi wa ‘kimya’en_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Edwell Dzomba.pdf
Size:
168.55 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: