Mchomozo wa kipragmatiki katika nagona na mzingile: uchunguzi wa ‘kimya’
Loading...
Date
2018
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza kimya kama mchomozo wa kipragmatiki katika riwaya mbili za Euphrase Kezilahabi ambazo ni Nagona na Mzingile. Mtafiti alikusanya data kwa kutumia mbinu ya usomaji matini. Sehemu zote zilizoandikwa neon ‘kimya’ na taarifa zinazozunguka neon hilo zilikusanywa kama data za kufanyia utafiti katika mazungumzo ya wahusika. Kila kimya kilipewa alama na kasha kikachambuliwa kwa kutumia mkabala wa kielimu-mitindo. Data zilichambuliwa kwa kutumia Mkabala wa kielimu-mtindo na Mkabala wa Korasi katika fasihi ambapo misingi ya Nadharia ya Uhusisho ya Sperber na Wilson (1986, 1995) na Nadharia ya Korasi katika Fasihi ya Mutembei (2012) imeunganishwa kuchunguza data. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, kimya katika riwaya za Kiswahili ni jambo la msingi na linahitaji umakini katika kuchunguza fani na maudhui ya riwaya za Kiswahili. Aidha, utafiti huu uligundua kuwa elimu-mtindo ni njia ya kipekee inayoweza kubainisha mtindo wa mwandishi kwa kina. Kupitia Mkabala wa Elimu-mitindo, kazi hii iliweza kuibua mtindo wa Kezilahabi katika matumizi ya kimya kuwasilisha mawazo yake. Kwa kuwa, kimya kinawasilisha mawazo yake. Kwa kuwa, kimya kinawasilisha maana iliyofichika na isiyo ya moja kwa moja, mkabala wa kielimu-mtindo umetumika kuchunguza mtindo wa Kezilahabi wa kumtaka msomaji aingilie kazi kwa undani kupitia matumizi ya kimya. Mkabala huu umeoneshwa na kufafanuaa maana zinazowasilishwa katika kimya hicho. Kwa hiyo, kuna haja ya kuchunguza kimya katika riwaya zingine za Kiswahili kwa kutumia mkabala na nadharia za kielimu-mitindo ili kuweza kubaini namna waandishi wanavyokitumia kuwasilisha maudhui yao katika mitindo mbalimbali.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.Z5.T34D964 )
Keywords
Language and languages, Swahili literature, Folk literrature, Kiswahili
Citation
Dzomba, E. (2018) Mchomozo wa kipragmatiki katika nagona na mzingile: uchunguzi wa ‘kimya’, Master dissertation, University of Dar es Salaam