Toni Katika Vitenzi Vya Lugha

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Tasnifu hii ni zao la utafiti uliochunguza utokeaji wa ‘’Toni katika vitenzi vya lugha ya Giha’’. Tafiti zilizokwisha kufanyika katika lugha ya Giha zinabainisha kuwa lugha hii ina toni. Pamoja na kubainisha hivyo, tafiti hizo hazikubainisha kiimbotoni msingi cha lugha hii wala kufafanua silabi inayohusishwa na kiinitoni. Aidha tafiti hizo hazikueleza kanuni mbalimbali za kitoni ambazo zinazojitokeza katika luwaza ya Toni. Utafiti huuu umejikita katika kuziba pengo Hilo. Katika kuziba pengo hili, tunajenga hoja kwamba ruwaza ya Toni katika vitenzi vya lugha ya Giha huanza na tonichini, kisha tonijuu na kuishia na tonichini tena. Kwa maana hyo, Kiimbotoni Msingi cha lugha ya Giha ni Chini Juu Chini (CJC). Aidha Katya lugha hii kiinitoni kinahusishwa na tonichini ya upande wa kushoto katika kiimbotoni msingi.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8228.6.B52)
Keywords
Ha language, Kigoma, Tanzania
Citation
Bichwa, Sail Simon (2016) Toni Katika Vitenzi Vya Lugha, Masters dissertation, University of Dar es Salaam