Dhima ya nyimbo katika ngano za jamii ya Wahehe

dc.contributor.authorMsigala, Deus Titus
dc.date.accessioned2019-11-25T13:19:22Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:49Z
dc.date.available2019-11-25T13:19:22Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:49Z
dc.date.issued2015
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8025.T34M73334)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umejadili dhima ya nyimbo katika ngano za jamii ya Wahehe. Tatizo lililojenga utafiti huu kuwa matini mbalimbali huingiliana na mwingiliano huo huwa na dhima mahususi. Matini husika zinapoingiliana huwa zinakamilishana na kushirikiana katika uwasilishaji wa maudhui. Kwa hiyo utafiti huu ulijikita kuchunguza dhima ya mwingiliano wa nyimbo na ngano. Ili kufanya hilo, tulichunguza dhima za nyimbo katika ngano za jamii ya Wahehe. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani na uwandani kwa kuchunguza nyimbo zinazojitokeza katika ngano nyingi ili kupata dhima ya jumla kuhusu nafasi ya nyimbo wakati wa utendaji ngano. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Mwingiliano matini; na umebaini kuwa nyimbo zina dhima kubwa katika ngano za Kihehe, tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa kuwa nyimbo hazina dhima yoyote zaidi ya kufurahisha. Kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa nyimbo katika ngano zina dhima kimaudhui na kifani. Kimaudhui dhima zilizogunduliwa ni kama vile kuibua dhamira, kubainisha migogoro, kubainisha falsafa ya jamii, kuleta uhalisia, kuibua hisia na kuhifadhi ngano. Kwa upande wa kifani dhima zilizoibuliwa ni kama vile kuleta usikivu, kuizindua hadhira, kuleta ushiriki wa hadhira, kutambulisha hadhira, kuondoa ukinaifu na kuongeza uhai wa ngano katika usimulizi. Mwisho utafiti huu umedokeza maeneo mengine ambayo yanatakiwa kufanyiwa utafiti zaidi yakiwamo ya kuchunguza dhima ya semi, methali na nahau katika ngano za jamii ya Wahehe.en_US
dc.identifier.citationMsigala, D.T. (2015) Dhima ya nyimbo katika ngano za jamii ya Wahehe, Tasnifu ya Uzamili (Kiswahili), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3530
dc.language.isootheren_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dar es Salaamen_US
dc.subjectHehe languageen_US
dc.subjectHehe (African people)en_US
dc.subjectSongsen_US
dc.titleDhima ya nyimbo katika ngano za jamii ya Waheheen_US
dc.typeThesisen_US

Files