Dhima ya nyimbo katika ngano za jamii ya Wahehe

No Thumbnail Available
Date
2015
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umejadili dhima ya nyimbo katika ngano za jamii ya Wahehe. Tatizo lililojenga utafiti huu kuwa matini mbalimbali huingiliana na mwingiliano huo huwa na dhima mahususi. Matini husika zinapoingiliana huwa zinakamilishana na kushirikiana katika uwasilishaji wa maudhui. Kwa hiyo utafiti huu ulijikita kuchunguza dhima ya mwingiliano wa nyimbo na ngano. Ili kufanya hilo, tulichunguza dhima za nyimbo katika ngano za jamii ya Wahehe. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani na uwandani kwa kuchunguza nyimbo zinazojitokeza katika ngano nyingi ili kupata dhima ya jumla kuhusu nafasi ya nyimbo wakati wa utendaji ngano. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Mwingiliano matini; na umebaini kuwa nyimbo zina dhima kubwa katika ngano za Kihehe, tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa kuwa nyimbo hazina dhima yoyote zaidi ya kufurahisha. Kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa nyimbo katika ngano zina dhima kimaudhui na kifani. Kimaudhui dhima zilizogunduliwa ni kama vile kuibua dhamira, kubainisha migogoro, kubainisha falsafa ya jamii, kuleta uhalisia, kuibua hisia na kuhifadhi ngano. Kwa upande wa kifani dhima zilizoibuliwa ni kama vile kuleta usikivu, kuizindua hadhira, kuleta ushiriki wa hadhira, kutambulisha hadhira, kuondoa ukinaifu na kuongeza uhai wa ngano katika usimulizi. Mwisho utafiti huu umedokeza maeneo mengine ambayo yanatakiwa kufanyiwa utafiti zaidi yakiwamo ya kuchunguza dhima ya semi, methali na nahau katika ngano za jamii ya Wahehe.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8025.T34M73334)
Keywords
Hehe language, Hehe (African people), Songs
Citation
Msigala, D.T. (2015) Dhima ya nyimbo katika ngano za jamii ya Wahehe, Tasnifu ya Uzamili (Kiswahili), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam