Usimulizi katika riwaya ya dunia uwanja wa fujo
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Riwaya za Euphrase Kezilahabai , Rosa Mistika (1971), Kichwa Maji (1974), Dunia Ilwanja wa Pio (1975), Gainful kl Nyoka (1979), Nagona (1990) na Mzingile (1991), zimewavutia wataalamu wengi kuzifanyia uchambuzi na utafiti. Miongoni mwa wataalamu hao ni Senkoro (1982, 2011), Mulokozi (1983), Wamitila (1997), na Sakkos (2008). Katika uchambuzi wao, wataalamu hao wamejikita zaidi katika kuchunguza dhamira, falsafa, motifu na kadhalika. Pamoja na kuzua mijadala kutokana na uchambuzi, riwaya hizo hazijafanyiwa uchambuzi wa kutosha kwa kuzingatia sifa zake za kiusimulizi. Hivyo, kwa kutumia nadharia ya usimulizi, tasinifu hii inachunguza suala la usimulizi kwa kuzingatia mbinu zake za usimulizi: wahusika na msimulizi. Hoja ya msingi ya tasinifu hii ni kuwa mbinu za usawiri wa wahusika na dhima ya msimulizi ni vipengele vinavyosaidia kubaini maudhui na malengo ya kazi inayohusika. Katika kuchunguza vipengele hivyo, tumejiuliza: Mbinu zipi zimetumika kuwajenga wahusika katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo? Zaidi ya kusimulia, msimulizi ana dhima nyingine? Kama ipo ni ipi? Kwa jumla, katika tasinifu hii mbinu mbalimbali za usawiri wa wahusika pamoja na dhima za msimulizi zimebainishwa na kufafanuliwa. Zaidi ya kubainishwa kwa mambo kayo, pia kumetolewa hitimisho la tasinifu na mapendekezo ya maeneo yanayohitaji kutafitiwa zaidi.