Uainishaji wa mbazi katika fasihi simulizi ya Kiswahili Mifano kutoka mbazi teule za kiha

dc.contributor.authorNzababa, David Edward
dc.date.accessioned2022-05-12T09:01:59Z
dc.date.available2022-05-12T09:01:59Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionAvailable in print form, Eat Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,(THS EAF PL8704.T34.N922 )en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kuchunguza uainishaji wa mbazi katika fasihi simulizi ya Kiswahili ukitumia mifano kutoka mbazi teule za Kiha .Lengo kuu la utafiti huu ilikuwa kuchunguza nafasi ya kigezo cha nduni bainifu katika uainishaji wa mbazi za kiha na fasihi simulizi ya Kiswahili kwa ujumla. Aidha malengo mahususi yalikuwa (i)Kupambanua nduni bainifu zinazojenga ujumi wa mbazi za Kiha (ii)Kuainisha mbazi za Kiha katika tanzu vipare na kumbo mahususi kulingana na nduni zake bainifu na(iii) kuonesha nafasi ya kigezo cha nduni bainifu kaika uainishaji wa mbazi za Kiha na fasihi simulizi ya kiswahili kwa ujumla.Data hizo zilichambuliwa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Tanzu iliyoasisiwa na wanafalsafa wa Kigiriki hususani plato na Aristotle.Isitoshe data hizo zilichambuliwa na mihimili miwili ya nadharia hii yaani mhimili wa nduni bainifu na mhimili wa kijamii.Aidha data za utafiti huu zilikusanywa uwandani kupitia mbinu za usaili na ushuhudiaji.Matokeo ya utaiti huu yanaonyesha kuwa mbazi ni kipera cha utanzu wa hadithi. Pia kupitia kigezo cha nduni bainifu utafiti huu ulibaini kuwapo kwa kumbo 11. kumbo hizo zimejumuisha mbazi za ulinganuzi mahususi,viumbe nasaha kinzani,wanadamu, usuluhishi,kuhamasisha jumla.kiishara na mbazi za kimethali .Halikadhalika utafiti huu umebaini kuwa kigezo chan duni bainifu kina manufaa makubwa katika kufanikisha uainishaji wa tanzu vipera na kumbo mahususi za mbazi. Isitoshe utafiti huu umebaini kuwa mchakato wa uainishaji wa umewasilisha dhima kubwa kitaaluma ikiwa ni pamoja na kuondoa mgongano uliokuwepo kuhusu nafasi ya kipera cha mbazi. Mgongano wa nafasi ya mbazi uliondolewa kupitia matokeo ya utafiti huu yaliyobainisha kuwa mbazi ni kipera cha utanzu wa hadithi kutokana na mfungamano mkubwa uliopo kati ya utanzu wa hadithi na mbazi katika nduni zake bainifu .Pia uainishaji umerahisisha ufundishaji wa fasihi simulizi kutokana na kupangiliwa mbazi katika mfumo wa nduni bainifu utanzu. kipera na kumbo .Mfumo huo unasaidia kujenga mantiki kwa mwalimu anayefundisha mbazi na kuwa mwanafunzi anayejifunza fasihi simulizi hususan kipera cha mbazi. Kadhalika tafiti nyingine zinaweza kuchunguza uainishaji wa mbazi kwa kuzingatia vigezo vingine vya uainishaji tofauti na kigezo cha nduni bainifu kilichozingatiwa katika utfiti huu .Utafiti huu umewafaa wanafunzi na wanazuoni kwa kuwa unaongeza maarifa kuhusu uainishaji katika fasihi simulizi ya Kiswahilien_US
dc.identifier.citationNzababa, D. E.(2019) Uainishaji wa mbazi katika fasihi simulizi ya Kiswahili Mifano kutoka mbazi teule za kihatasnifu ya MA(kiswahili). Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.172.12:8090/xmlui/handle/123456789/16607
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectStory tellingen_US
dc.subjectKihaen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleUainishaji wa mbazi katika fasihi simulizi ya Kiswahili Mifano kutoka mbazi teule za kihaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
nzababa.pdf
Size:
177.94 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: