Uainishaji wa mbazi katika fasihi simulizi ya Kiswahili Mifano kutoka mbazi teule za kiha

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es salaam
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza uainishaji wa mbazi katika fasihi simulizi ya Kiswahili ukitumia mifano kutoka mbazi teule za Kiha .Lengo kuu la utafiti huu ilikuwa kuchunguza nafasi ya kigezo cha nduni bainifu katika uainishaji wa mbazi za kiha na fasihi simulizi ya Kiswahili kwa ujumla. Aidha malengo mahususi yalikuwa (i)Kupambanua nduni bainifu zinazojenga ujumi wa mbazi za Kiha (ii)Kuainisha mbazi za Kiha katika tanzu vipare na kumbo mahususi kulingana na nduni zake bainifu na(iii) kuonesha nafasi ya kigezo cha nduni bainifu kaika uainishaji wa mbazi za Kiha na fasihi simulizi ya kiswahili kwa ujumla.Data hizo zilichambuliwa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Tanzu iliyoasisiwa na wanafalsafa wa Kigiriki hususani plato na Aristotle.Isitoshe data hizo zilichambuliwa na mihimili miwili ya nadharia hii yaani mhimili wa nduni bainifu na mhimili wa kijamii.Aidha data za utafiti huu zilikusanywa uwandani kupitia mbinu za usaili na ushuhudiaji.Matokeo ya utaiti huu yanaonyesha kuwa mbazi ni kipera cha utanzu wa hadithi. Pia kupitia kigezo cha nduni bainifu utafiti huu ulibaini kuwapo kwa kumbo 11. kumbo hizo zimejumuisha mbazi za ulinganuzi mahususi,viumbe nasaha kinzani,wanadamu, usuluhishi,kuhamasisha jumla.kiishara na mbazi za kimethali .Halikadhalika utafiti huu umebaini kuwa kigezo chan duni bainifu kina manufaa makubwa katika kufanikisha uainishaji wa tanzu vipera na kumbo mahususi za mbazi. Isitoshe utafiti huu umebaini kuwa mchakato wa uainishaji wa umewasilisha dhima kubwa kitaaluma ikiwa ni pamoja na kuondoa mgongano uliokuwepo kuhusu nafasi ya kipera cha mbazi. Mgongano wa nafasi ya mbazi uliondolewa kupitia matokeo ya utafiti huu yaliyobainisha kuwa mbazi ni kipera cha utanzu wa hadithi kutokana na mfungamano mkubwa uliopo kati ya utanzu wa hadithi na mbazi katika nduni zake bainifu .Pia uainishaji umerahisisha ufundishaji wa fasihi simulizi kutokana na kupangiliwa mbazi katika mfumo wa nduni bainifu utanzu. kipera na kumbo .Mfumo huo unasaidia kujenga mantiki kwa mwalimu anayefundisha mbazi na kuwa mwanafunzi anayejifunza fasihi simulizi hususan kipera cha mbazi. Kadhalika tafiti nyingine zinaweza kuchunguza uainishaji wa mbazi kwa kuzingatia vigezo vingine vya uainishaji tofauti na kigezo cha nduni bainifu kilichozingatiwa katika utfiti huu .Utafiti huu umewafaa wanafunzi na wanazuoni kwa kuwa unaongeza maarifa kuhusu uainishaji katika fasihi simulizi ya Kiswahili
Description
Available in print form, Eat Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,(THS EAF PL8704.T34.N922 )
Keywords
Swahili literature, Story telling, Kiha, Tanzania
Citation
Nzababa, D. E.(2019) Uainishaji wa mbazi katika fasihi simulizi ya Kiswahili Mifano kutoka mbazi teule za kihatasnifu ya MA(kiswahili). Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.