Usawiri wa ontolojia ya kiafrika katika ngano za Kiha.

dc.contributor.authorRaphael, Deogratias
dc.date.accessioned2020-04-19T19:31:14Z
dc.date.available2020-04-19T19:31:14Z
dc.date.issued2018
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8025.T34R36)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umejadili vipengele vya Ontolojia ya Kiafrika vinavyosawiriwa katika ngano za Kiha. Tatizo lililosukuma utafiti huu ni kuwapo kwa makundi mawili yanayojadili Ontolojia ya Kiafrika kwa kujikita katika dini na masuala ya kijamii, kiutamaduni na mahusiano ya kiutawala bila kuhusisha fasihi. Kwa hiyo, utafiti huu ulijikita katika ngano za Waha ili kuona namna zinavyosawiri Ontolojia ya Kiafrika. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza usawiri wa Ontolojia ya Kiafrika katika ngano za Kiha. Malengo mahususi yalikuwa kubainisha vipengele vya Ontolojia ya Kiafrika katika ngano za kiha na kujadili namna Ontolojia ya Kiafrika inavyosawiriwa katika ngano za Kiha. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika inahusu masuala ya maisha na dhima ya kuwapo kwake. Msisitizo wa nadharia hii ni mahusiano yaliyopo baina ya ulimwengu katika nyuga tatu na walimwengu waliomo katika nyuga hizo. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani na uwandani kuchunguza ngano zilizokusanywa katika vijiji vitano (Janda, Kirungu, Kimara, Kinazi na Munzeze) vya wilaya ya Buhigwe zinavyosawiri Ontolojia ya Kiafrika. Ngano zilikusanywa, kufasiriwa na kuchambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli. Watafitiwa walikuwa ni mchanganyiko wa wanawake na wanaume wa umri tofautitofauti. Wazee wenye ufahamu wa mila na desturi za Waha walihusishwa katika uchambuzi wa ngano zilizohakikiwa. Kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa ngano zinasawiri Ontolojia ya Kiafrika. Vipengele mbalimbali vya Ontolojia ya Kiafrika vimebainishwa katika utafiti huu. Vipengele hivyo ni pamoja na uduara wa maisha, dhana ya kifo, kuwapo kwa Mungu Mkuu, matambiko, imani katika sihiri na uganga, uzazi, ndoa na malezi, miiko, familia pana, mizimu na mapepo, utoaji wa majina, usababishi/sababu ya matukio na dhana ya wakati. Vipengele vingine ni kuwapo kwa nguvu zilizo nje ya mazingira ya kawaida, kuwapo kwa maisha baada ya kufa, roho kuhamia katika kiumbe kingine, umoja na mshikamano na maadili/tabia njema. Utafiti huu umeonesha kwamba ngano zinaweza kubeba ontolojia ya jamii bila kujiegemeza katika dini au masuala ya kijamii kama vile siasa na uchumi. Msuko wa visa na matukio katika ngano umeweza kudhihirisha uontolojia uliomo katika ngano hizo.en_US
dc.identifier.citationRaphael, D. (2018). Usawiri wa ontolojia ya kiafrika katika ngano za Kiha. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/9604
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectBantu languagesen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectNgano za kihaen_US
dc.titleUsawiri wa ontolojia ya kiafrika katika ngano za Kiha.en_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Raphael 2018.pdf
Size:
178.88 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: