Usawiri wa mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijimsia katika fasihi picha ya katuni mnato za kiswahili

dc.contributor.authorChaligha, Elizaberth N
dc.date.accessioned2021-02-10T10:29:12Z
dc.date.available2021-02-10T10:29:12Z
dc.date.issued2011
dc.descriptionAvailable in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8704.C4752)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umejadili kuhusu usawiri wa mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijinsia katika fasihi picha ya katuni mnato za Kiswahili. Tatizo lililojenga utafiti huu ni kutokana na hali ya kila siku ya uchoraji wa katuni katika magazeti, majarida na katika wavuti ambazo humkweza mwanaume kinafasi na kimajukumu na kumshusha mwanamke, hivyo utafiti huu ulijikita kuchunguza nafasi ya mwanamke katika fasihi picha ya katuni mnato za Kiswahili. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani kwa kuchunguza katuni nyingi ili kupata ruwaza ya jumla kuhusu nafasi ya mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijinsia. Pia umeongozwa na nadharia mbili-nadharia ya ufeministi na nadharia ya ucheshi. Hivyo utafiti huu umebaini kuwa kuna tofauti kubwa za kimajukumu kati ya mwanaume na mwanamke, kwani mwanamke amesawiriwa kwa mtazamo hasi yaani ameonekana ni kiumbe duni,mnyonge na hivyo kuendelea kumdharau, kumkejeli na kumdhihaki. Hivyo basi kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa katika jamii nafasi ya mwanamke na mgawanyo wa majukumu huwa tofauti na mwanaume kwa sababu ya mila na tamaduni mbovu ambazo humchukulia mwanamke kama kiumbe duni wakati wote ingawa uhalisia wa sasa hauko hivyo. Utafiti huu umependekeza kuwa jamii inapaswa kumswiri mwanamke kama kiumbe shupavu, mwenye mtazamo wa kujenga na kuiendeleza jamii, kwa hiyo kuwe na mgawanyo sawa wa majukumu. Mwisho utafiti umedokeza maeneo mengine ambayo yanatakiwa kufanyiwa utafiti zaidi; kumchambua mwanakatuni mmoja mmoja ili kujua falsafa yake katika fasihi picha ya katuni, na kutafiti vipengele vya fani na maudhuien_US
dc.identifier.citationChaligha, Elizaberth N (2011) Usawiri wa mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijimsia katika fasihi picha ya katuni mnato za kiswahilien_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/14710
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectCartoonsen_US
dc.subjectCaricatures and Cartoonsen_US
dc.subjectWomenen_US
dc.titleUsawiri wa mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijimsia katika fasihi picha ya katuni mnato za kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Elizaberth Nathaniel Chaligha.pdf
Size:
5.17 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: