Usawiri wa mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijimsia katika fasihi picha ya katuni mnato za kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umejadili kuhusu usawiri wa mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijinsia katika fasihi picha ya katuni mnato za Kiswahili. Tatizo lililojenga utafiti huu ni kutokana na hali ya kila siku ya uchoraji wa katuni katika magazeti, majarida na katika wavuti ambazo humkweza mwanaume kinafasi na kimajukumu na kumshusha mwanamke, hivyo utafiti huu ulijikita kuchunguza nafasi ya mwanamke katika fasihi picha ya katuni mnato za Kiswahili. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani kwa kuchunguza katuni nyingi ili kupata ruwaza ya jumla kuhusu nafasi ya mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijinsia. Pia umeongozwa na nadharia mbili-nadharia ya ufeministi na nadharia ya ucheshi. Hivyo utafiti huu umebaini kuwa kuna tofauti kubwa za kimajukumu kati ya mwanaume na mwanamke, kwani mwanamke amesawiriwa kwa mtazamo hasi yaani ameonekana ni kiumbe duni,mnyonge na hivyo kuendelea kumdharau, kumkejeli na kumdhihaki. Hivyo basi kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa katika jamii nafasi ya mwanamke na mgawanyo wa majukumu huwa tofauti na mwanaume kwa sababu ya mila na tamaduni mbovu ambazo humchukulia mwanamke kama kiumbe duni wakati wote ingawa uhalisia wa sasa hauko hivyo. Utafiti huu umependekeza kuwa jamii inapaswa kumswiri mwanamke kama kiumbe shupavu, mwenye mtazamo wa kujenga na kuiendeleza jamii, kwa hiyo kuwe na mgawanyo sawa wa majukumu. Mwisho utafiti umedokeza maeneo mengine ambayo yanatakiwa kufanyiwa utafiti zaidi; kumchambua mwanakatuni mmoja mmoja ili kujua falsafa yake katika fasihi picha ya katuni, na kutafiti vipengele vya fani na maudhui
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8704.C4752)
Keywords
Swahili literature, Cartoons, Caricatures and Cartoons, Women
Citation
Chaligha, Elizaberth N (2011) Usawiri wa mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijimsia katika fasihi picha ya katuni mnato za kiswahili