Matumizi ya majina ya asili ya familia na utambulisho wa jamii ya Wanyakyusa

dc.contributor.authorKategela, Rose
dc.date.accessioned2019-11-12T11:05:43Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:46Z
dc.date.available2019-11-12T11:05:43Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:46Z
dc.date.issued2013
dc.description.abstractUtafiti huu umechunguza Matumizi ya Majina ya Asili ya Familia na Utambulisho wa Jamii ya Wanyakyusa. Utafiti ulilenga kuainisha majina ya asili ya familia ya Wanyakyusa kwa kuzingatia asili ya majina hayo; kueleza vigezo vinavyotumiwa kutoa majina ya asili ya familia kwa jamii ya Wanyakyusa, na kuchambua maumbo ya majina ya asili ya familia yanayotambulisha jamii ya Wanyakyusa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utambulisho wa kijamii ya Tajfel (1982). Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka vijiji vya Ilolo na Segela vilivyoko katika kata za Kiwira na Bujela katika wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya. Utafiti ulihusisha sampuli ya watafitiwa 40 ambapo usampulishaji nasibu tabakishi ulitumika kwa kutumia kigezo cha umri. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji, mahojiano na hifadhi ya maandishi na kisha kufafanuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa majina yaliyotumika katika utafiti huu, yameainishwa katika aina tatu: majina yanayotolewa wakati wa kuzaliwa mtoto, majina yanayotolewa wakati wa ubatizo na majina ya utani. Utafiti umebaini kuwa kuna vigezo vinane vinavyozingatiwa wakati wa kutoa majina. Vigezo hivyo ni namna mtoto alivyozaliwa, mahali mtoto alipozaliwa, muda na kipindi ambacho mtoto alizaliwa, hali ya ujauzito na matatizo ya uzazi uliotangulia, mfuatano wa watoto, hali ya kiuchumi ya familia, kurithi jina la mtu mwingine na kuzingatia aina ya jinsi. Vilevile, utafiti umedhihirisha maumbo yanayotambulisha jamii ya Wanyakyusa kuwa ni maumbo ya majina ya asili ya lugha ya Kinyakyusa yatokanayo na uambatizi, unyambuzi wa vitenzi, uambatani/muambatano, maumbo ya vitenzi mashina na maumbo ya nomino huru.en_US
dc.identifier.citationKategela, R (2013) Matumizi ya majina ya asili ya familia na utambulisho wa jamii ya Wanyakyusa, Tasinifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3509
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectNyakyusa (African people)en_US
dc.subjectNyakyusa languageen_US
dc.subjectNamesen_US
dc.subjectNyakyusaen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleMatumizi ya majina ya asili ya familia na utambulisho wa jamii ya Wanyakyusaen_US
dc.typeThesisen_US
Files