Matumizi ya majina ya asili ya familia na utambulisho wa jamii ya Wanyakyusa

No Thumbnail Available
Date
2013
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza Matumizi ya Majina ya Asili ya Familia na Utambulisho wa Jamii ya Wanyakyusa. Utafiti ulilenga kuainisha majina ya asili ya familia ya Wanyakyusa kwa kuzingatia asili ya majina hayo; kueleza vigezo vinavyotumiwa kutoa majina ya asili ya familia kwa jamii ya Wanyakyusa, na kuchambua maumbo ya majina ya asili ya familia yanayotambulisha jamii ya Wanyakyusa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utambulisho wa kijamii ya Tajfel (1982). Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka vijiji vya Ilolo na Segela vilivyoko katika kata za Kiwira na Bujela katika wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya. Utafiti ulihusisha sampuli ya watafitiwa 40 ambapo usampulishaji nasibu tabakishi ulitumika kwa kutumia kigezo cha umri. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji, mahojiano na hifadhi ya maandishi na kisha kufafanuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa majina yaliyotumika katika utafiti huu, yameainishwa katika aina tatu: majina yanayotolewa wakati wa kuzaliwa mtoto, majina yanayotolewa wakati wa ubatizo na majina ya utani. Utafiti umebaini kuwa kuna vigezo vinane vinavyozingatiwa wakati wa kutoa majina. Vigezo hivyo ni namna mtoto alivyozaliwa, mahali mtoto alipozaliwa, muda na kipindi ambacho mtoto alizaliwa, hali ya ujauzito na matatizo ya uzazi uliotangulia, mfuatano wa watoto, hali ya kiuchumi ya familia, kurithi jina la mtu mwingine na kuzingatia aina ya jinsi. Vilevile, utafiti umedhihirisha maumbo yanayotambulisha jamii ya Wanyakyusa kuwa ni maumbo ya majina ya asili ya lugha ya Kinyakyusa yatokanayo na uambatizi, unyambuzi wa vitenzi, uambatani/muambatano, maumbo ya vitenzi mashina na maumbo ya nomino huru.
Description
Keywords
Nyakyusa (African people), Nyakyusa language, Names, Nyakyusa, Tanzania
Citation
Kategela, R (2013) Matumizi ya majina ya asili ya familia na utambulisho wa jamii ya Wanyakyusa, Tasinifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)