Matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es salaam

dc.contributor.authorPeterson, Rhoda
dc.date.accessioned2019-11-27T06:35:13Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:50Z
dc.date.available2019-11-27T06:35:13Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:50Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF LB1139.L3T34P6)en_US
dc.description.abstractShauku ya kuchunguza eneo la mandhari-lugha inaendelea kukua miongoni mwa watafiti wa lugha kutokana na kushamiri kwa maandishi katika sehemu za wazi. Ulinganishaji wa maandishi binafsi na ya kiserikali umekuwa kama msingi wa tafiti za kimandhari-lugha. Kigezo hiki pekee hakiakisi matumizi halisi ya lugha katika eneo hilo kwani linahusisha shughuli tofauti za kijamii. Utafiti huu wa matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es Salaam umefanywa kwa kuzingatia muktadha wa kibiashara. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya semiotiki-jamii ya Halliday inayochunguza lugha kwa kuihusisha na jamii. Data zilizoko kwenye mfumo wa kongoo-andishi zilikusanywa kwa njia ya kupiga picha. Ushuhudiaji wa huduma zitolewazo madukani na mahojiano kwa wafanyabiashara zilikuwa njia za nyongeza za ukusanyaji wa data. Ufafanuzi wa data ulifanywa kwa kutumia njia ya uchambuzi mada. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa Dar es Salaam ni jiji lenye matumizi ya wingilugha. Lugha zilizobainika kutumiwa ni Kiingereza, Kiswahili, lugha za asili, Kiarabu, Kichina, Kihindi, na Kikorea. Lugha ya Kiingereza inatawala kimatumizi ikifuatiwa na Kiswahili, kisha lugha zingine zimetumiwa kwa kiasi kidogo sana. Dhima za lugha zilizodhihirika ni kukaribisha na kushawishi wateja wanunue bidhaa, kutambulisha bidhaa, jamii mbalimbali na imani za kidini. Kutokana na data za utafiti huu inapendekezwa kwamba muktadha wa matumizi ni kipengele kingine kinachoweza kutumiwa kuchunguza matumizi ya lugha katika mandhari-lugha. Vilevile, maudhui ni kipengele kinachoweza kutumiwa kuchunguza dhima za lugha katika mandhari-lugha.en_US
dc.identifier.citationPeterson, R. (2014) Matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es salaam, Doctoral dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3541
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectMedium of instructionen_US
dc.subjectLanguage Study and teachingen_US
dc.subjectSecondary educationen_US
dc.subjectPolicy makingen_US
dc.titleMatumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es salaamen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Collections