Matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es salaam

No Thumbnail Available
Date
2014
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Shauku ya kuchunguza eneo la mandhari-lugha inaendelea kukua miongoni mwa watafiti wa lugha kutokana na kushamiri kwa maandishi katika sehemu za wazi. Ulinganishaji wa maandishi binafsi na ya kiserikali umekuwa kama msingi wa tafiti za kimandhari-lugha. Kigezo hiki pekee hakiakisi matumizi halisi ya lugha katika eneo hilo kwani linahusisha shughuli tofauti za kijamii. Utafiti huu wa matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es Salaam umefanywa kwa kuzingatia muktadha wa kibiashara. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya semiotiki-jamii ya Halliday inayochunguza lugha kwa kuihusisha na jamii. Data zilizoko kwenye mfumo wa kongoo-andishi zilikusanywa kwa njia ya kupiga picha. Ushuhudiaji wa huduma zitolewazo madukani na mahojiano kwa wafanyabiashara zilikuwa njia za nyongeza za ukusanyaji wa data. Ufafanuzi wa data ulifanywa kwa kutumia njia ya uchambuzi mada. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa Dar es Salaam ni jiji lenye matumizi ya wingilugha. Lugha zilizobainika kutumiwa ni Kiingereza, Kiswahili, lugha za asili, Kiarabu, Kichina, Kihindi, na Kikorea. Lugha ya Kiingereza inatawala kimatumizi ikifuatiwa na Kiswahili, kisha lugha zingine zimetumiwa kwa kiasi kidogo sana. Dhima za lugha zilizodhihirika ni kukaribisha na kushawishi wateja wanunue bidhaa, kutambulisha bidhaa, jamii mbalimbali na imani za kidini. Kutokana na data za utafiti huu inapendekezwa kwamba muktadha wa matumizi ni kipengele kingine kinachoweza kutumiwa kuchunguza matumizi ya lugha katika mandhari-lugha. Vilevile, maudhui ni kipengele kinachoweza kutumiwa kuchunguza dhima za lugha katika mandhari-lugha.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF LB1139.L3T34P6)
Keywords
Medium of instruction, Language Study and teaching, Secondary education, Policy making
Citation
Peterson, R. (2014) Matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es salaam, Doctoral dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.
Collections