Dhima ya ucheshi katika kuibua visa na maudhui: uchambuzi wa riwaya ya marimba ya majaliwa

dc.contributor.authorMwaijande, Gwantwa
dc.date.accessioned2019-07-22T14:39:56Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:39Z
dc.date.available2019-07-22T14:39:56Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:39Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionAvailable in print formen_US
dc.description.abstractUcheshi ni tabia ya kuwa mchangamfu na mwenye furaha kwa watu. Ni mbinu ya kifani inayotumiwa na wasanii katika kutimiza malengo yao ya uandishi. Baadhi ya faida za ucheshi ni kuondoa uchovu, kuburudisha na kusaidia kujenga taswira. Kazi hii imechunguza Dhima ya Ucheshi katika Kuibua Visa na Maudhui: Uchambuzi wa Riwaya ya Marimba ya Majaliwa. Malengo ya jumla ya utafiti huu yalikuwa ni kutafiti na kubainisha ucheshi na kuonesha jinsi ucheshi unavyoibua visa na unavyojenga maudhui katika riwaya ya Marimba ya Majaliwa. Ili kufanikisha utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu ya maktabani katika kukusanya na kuwasilisha data kimaelezo. Vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji wa data ni shajara, kalamu, kompyuta na kinyonyi. Vile vile marejeleo mbalimbali kutoka katika wavuti yalipitiwa. Nadharia ya Mwitikio wa Msomaji ndiyo iliyotumika katika kufanikisha utafiti huu. Nadharia hii imemsaidia mtafiti kuweza kubaini mawazo mbalimbali ya mwandishi katika riwaya yake ambayo ni aina za ucheshi, visa na maudhui yanayotokana na ucheshi kutoka katika riwaya ya Marimba ya Majaliwa. Kwa ujumla matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti kwani yalibainisha aina za ucheshi na dhima yake katika jamii. Dhima hizo za ucheshi ni kuburudisha, kuonya, kuelimisha na kuadibisha. Pia matokeo hayo ya utafiti yalibainisha visa vya msako wa marimba, mnyonge kumshinda mwenye nguvu na utundu na ubunifu. Visa vingine ni vya abiria safarini, tamaa ya binadamu na ndoto ya kikojozi. Maudhui yanayotokana na ucheshi kutoka katika riwaya ya Marimba ya Majaliwa yana mchango mkubwa katika fasihi kwa ujumla.en_US
dc.identifier.citationMwaijande, G. (2012) Dhima ya ucheshi katika kuibua visa na maudhui: uchambuzi wa riwaya ya marimba ya majaliwa. Master dissertation, University of Dar es Salaam, Avaialble athttp://41.86.178.3/internetserver3.1.2/search.aspx?formtype=advanceden_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3431
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectMarimba ya majaliwaen_US
dc.titleDhima ya ucheshi katika kuibua visa na maudhui: uchambuzi wa riwaya ya marimba ya majaliwaen_US
dc.typeThesisen_US

Files