Dhima ya ucheshi katika kuibua visa na maudhui: uchambuzi wa riwaya ya marimba ya majaliwa

No Thumbnail Available
Date
2012
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Ucheshi ni tabia ya kuwa mchangamfu na mwenye furaha kwa watu. Ni mbinu ya kifani inayotumiwa na wasanii katika kutimiza malengo yao ya uandishi. Baadhi ya faida za ucheshi ni kuondoa uchovu, kuburudisha na kusaidia kujenga taswira. Kazi hii imechunguza Dhima ya Ucheshi katika Kuibua Visa na Maudhui: Uchambuzi wa Riwaya ya Marimba ya Majaliwa. Malengo ya jumla ya utafiti huu yalikuwa ni kutafiti na kubainisha ucheshi na kuonesha jinsi ucheshi unavyoibua visa na unavyojenga maudhui katika riwaya ya Marimba ya Majaliwa. Ili kufanikisha utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu ya maktabani katika kukusanya na kuwasilisha data kimaelezo. Vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji wa data ni shajara, kalamu, kompyuta na kinyonyi. Vile vile marejeleo mbalimbali kutoka katika wavuti yalipitiwa. Nadharia ya Mwitikio wa Msomaji ndiyo iliyotumika katika kufanikisha utafiti huu. Nadharia hii imemsaidia mtafiti kuweza kubaini mawazo mbalimbali ya mwandishi katika riwaya yake ambayo ni aina za ucheshi, visa na maudhui yanayotokana na ucheshi kutoka katika riwaya ya Marimba ya Majaliwa. Kwa ujumla matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti kwani yalibainisha aina za ucheshi na dhima yake katika jamii. Dhima hizo za ucheshi ni kuburudisha, kuonya, kuelimisha na kuadibisha. Pia matokeo hayo ya utafiti yalibainisha visa vya msako wa marimba, mnyonge kumshinda mwenye nguvu na utundu na ubunifu. Visa vingine ni vya abiria safarini, tamaa ya binadamu na ndoto ya kikojozi. Maudhui yanayotokana na ucheshi kutoka katika riwaya ya Marimba ya Majaliwa yana mchango mkubwa katika fasihi kwa ujumla.
Description
Available in print form
Keywords
Swahili literature, Marimba ya majaliwa
Citation
Mwaijande, G. (2012) Dhima ya ucheshi katika kuibua visa na maudhui: uchambuzi wa riwaya ya marimba ya majaliwa. Master dissertation, University of Dar es Salaam, Avaialble athttp://41.86.178.3/internetserver3.1.2/search.aspx?formtype=advanced