Dhima ya nyimbo katika matambiko ya wazaramo

Date

2011

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu unahusu nyimbo za matambiko ya Wazaramo. Data na taarifa za utafiti zimekusanywa kutoka uwandani, na mbinu zilizotumika kukusanyia data ni mbinu za uchunguzi kifani, ushiriki, maktabani na mahojiano. Nadharia ya Semiotiki imetoa mwongozo katika uchambuzi wa nyimbo ishirini na tano tulizoziteua. Uchambuzi wa nyimbo hizo umeibua dhima mbalimbali zinazohusiana na nyimbo hizo. Muundo wa nyimbo hizo na mabadiliko yaliyojitokeza katika nyimbo hizo tangu zamani hadi sasa. Kwa jumla uchambuzi umebainisha kuwa nyimbo hizi zina dhima zenye mafundisho mema kwa jamii husika. Nyimbo hizi zina umuhimu mkubwa katika jamii ya Wazaramo. Vipengele vichache vya utumizi wa lugha vimejitokeza lakini hatukuvijadili. Mwisho hitimisho la jumla la utafiti mzima pamoja na mapendekezo ya maeneo yanayohitaji kutafitiwa zaidi yameonyeshwa.

Description

Available in print form

Keywords

Swahili language, Zaramo (African people)

Citation

Salehe, T. (2011) Dhima ya nyimbo katika matambiko ya wazaramo, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Avaialable at (http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/search.aspx?formtype=advanced)