Ulinganishi wa Kiisimu katika Lahaja za Ki- Ngonde na KI- Mwamba za lugha ya Kinyakyusa

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulikuwa ni mchakato wa kuchunguza mfanano na tofauti za kiisimu baina ya lahaja yak i-ngonde na ki-mwamba ili kuthibitisha kama ki-ngonde na ki-mwamba ni lahaja za lugha moja, ni lugha mbili tofauti au sio lahaja bali ni lugha moja tu. Utafiti huu umefanyika katika vijiji vya ndala na lugombo katika wilaya ya rungwe na vijiji vya ngeleka na makwale katika wilaya ya kyela katika mkoa wa mbeya. Mbinu za utafiti zilihusu usampulihaji na sampuli na mbinu za ukusanyaji data na mbinu za uchambuzi wa data. Data ya utafiti iliyohusika katika utafiti huu ni data ya kutoka uwandani ambapo maswali mbalimbali yaliulizwa ili kujazwa na watoa taarifa. Msamiati wa lugha ya Kiswahili uliteuliwa ili watoa taarifa waingize ulitumia pia data ya maktabani, (upitia maandiko, kazi hii imegawanyika katika sura ya tano. Sura ya kwanza inaeleza juu ya kiini cha tatizo na mbinu ambazo zimetumika katika kufikia mahitimisho. Sura ya pili imeshughulika mapitio mbalimbali ya maandiko yanayohusu lahaja katika lugha za kibantu ambazo zimewahi kuandikiwa. Sura ya tatu imejihusisha na kujadili mbinu za kukusanya data na mbinu zilizotumika kuchanganua data. Sura ya nne imeshughulikia uwasilishaji na uchanguzi wa data. Data za uwandani zimechanganuliwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Uchanganuzi huu wa data umeongozwa na nadharia ya isimu liunganishi na nadharia tete ya ndugu wa karibu na ndugu wa mbali ya nadharia ya makutano na mwachano. Sura ya tano imeshughulikia matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa ki-ngonde na ki-mwamba ni lahaja zinazokaribiana sana zenye tofauti ndogo ndogo sana. Kutokana na matokeo hayo tunahitimisha kuwa ki-ngonde na ki-mwamba ni lahaja za lugha ya kinyakyusa zenye tofauti ndogo ndogo.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8549.M8521)
Keywords
Ngondo language, Mwamba language, Nyakyusa language
Citation
Mwambapa, Elisha (2016) Ulinganishi wa Kiisimu katika Lahaja za Ki- Ngonde na KI- Mwamba za lugha ya Kinyakyusa, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam