Utaratibu Wa Utoaji Majina Ya Asili Na Maana Zake Katika Jamii Ya Masai

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu utaratibu wa utoaji majina ya asili na maana zake katika jamii ya mamaasai wanaoishi wilaya ya Arusha vijijini mkoa wa Arusha Tanzania. Utafiti unahusisha jumla ya watoa data 48 kutpka kata za Kiranyi, Oltument na Kisongo.Taarifa zimekusanywa kwa njia ya hojaji na mahojiano. Utafiti ulikusudia kufahamu utaratibu wa utoaji majina ya asili ya rika na ukoo pamoja na maana zake katika jamii ya wamaasai. Ili kutimiza malengo haya mikabala miwiliya klinadharia imetumika mabayo ni; Nadharia ya Makutano na Mwachano na Nadharia ya uimbaji, nadharia ya makutano na Mwachano imetumika kubainisha mazingira ya mkutano yyanayojidhihirisha katika jamii hii kuendelea kutoa majina ya rika kwa kuzingatia matukio ya kihistoria. Mkabala wa uumbaji umetumika kubainisha namna binadam anavyoweza kuuona ulimwengu kupitia taratibu zilizowekwa na lugha yake ya kwanza. Kwa msingi huo majina ya asili ya jamii ya wamaasai yanabeba historia ya jamii hyo. Utafiti huu umebaini kuwa katika jamii ya wamaasai majina ya rika hupewa jina jipya. Utoaji w majina ya rika kwa rika kwa kila hatua husaidia kuhimiza majukumu ya kijamii na mipaka ya kila rika ili kudumisha heshima na uwajibikaji katika jamii. Vilevile majina ya utani wa rikahutumika zaidi ili kutimiza historia ya jamii hiyo. Aidha, utaratibu wa utoaji majina ya ukoo nin wa kurithishana isipokuwa mtu aliruhusiiwa kubadili jina la ukoo kwa utaratibu wa kubadili chapa na alama kwenye masikio ya ng’ombe mbuzi au kondoo pamoja na kunyolewa nywele ili kuashiria kuachana na jina la awali
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8501.J63)
Keywords
Maasai language, Traditional names, Names
Citation
John, Samwel (2016) Utaratibu Wa Utoaji Majina Ya Asili Na Maana Zake Katika Jamii Ya Masai, Masters dissertation, University of Dar es Salaam