Fonolojia ya Kigweno.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umelenga kubainisha miundo ya silabi za Kigweno, michakato ya kifonolojia pamoja na athali zake katika konsonati na irabu za Kigweno. Katika utafiti huu tumetumia hojaji pamoja na kusikiliza mazungumzo ya wazawa kupata data ambapo watoa taarifa wasiopungua 60 kutoka vijiji vya Vuchama. Mangio, Mcheni na Mwaniko walishilikishwa. Nadharia iliyotuongoza Katika uchanganuzi wa data ni nadharia ya Umbo Upeo (UU) ambayo inaachana na matumizi ya kanuni na sheria na badala yake inatumia seti ya mashartizuizi ili kufikia upeo wa ukubalifu. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwa, kuna miundo minne ya silabi za Kigweno ambayo ni 1, K,KI na KKI. Tumebaini pia kuwa Kjgweno kina michakato kadhaa ya kifonolojia inayoathiri konsonanti na ile inayoathiri irabu. Inayoathiri irabu ni pamoja na Udondoshaji wa Irabu, Muungano wa irabu. Tangamano la irabu. Uchopekaji wa irabu, Unazalishaji wa irabu pamoja na kanuni ya Uyeyushali. Kwa upside wa michakato inayohusu konsonanti tumebaini kuwepo kwa usilimisho pamwe wa nazali.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8228.24C4752)
Keywords
Gweno language, Phonology
Citation
Charles, A. (2011). Fonolojia ya Kigweno. Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.