Usawiri wa mhusika mlevi katika riwaya teule za Kiswahili

dc.contributor.authorMagoma, John
dc.date.accessioned2020-04-07T14:30:21Z
dc.date.available2020-04-07T14:30:21Z
dc.date.issued2017
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.5.M33)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza Usawiri wa Mhusika Mlevi katika Riwaya Teule za Kiswahili ambazo ni Rosa Mistika (1971), Uwike Usiwike Kutakucha (1978), Ua la Faraja (2004) na Watoto wa Maman’tilie (2012). Utafiti umejadili vyanzo vya mhusika kuwa mlevi wa pombe na athari za mhusika mlevi wa pombe kama ilivyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa maktabani kwa kusoma na kuchambua riwaya teule za Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Saiko Changanuzi katika uchambuzi wa data. Utafiti huu umebainisha vyanzo vya mhusika kuwa mlevi wa pombe na athari za mhusika mlevi wa pombe kama ilivyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili. Baadhi ya vyanzo vya mhusika kuwa mlevi wa pombe vinavyobainishwa na riwaya teule ni pamoja na mhusika kutaka ushirika wa kijamii, kutaka kuonekana maarufu au kujulikana katika jamii, kutaka kuondoa mfadhaiko au wasiwasi na kukabiliana na changamoto za maisha. Aidha, athari za mhusika mlevi wa pombe ni kama vile, mhusika mlevi kuwa chanzo cha migogoro, vurugu, usumbufu na kero katika familia, kuiba fedha za mwenzi wake, kufuja fedha, kupoteza ajira, kuathiri mwili, kutelekeza familia, kujiingiza katika tabia hatarishi na kusababisha kifo. Hivyo, utafiti umeweka wazi namna usawiri wa mhusika mlevi katika riwaya teule za Kiswahili unavyolenga kuitahadharisha jamii kuhusu athari hasi za aina mbalimbali zinazosababishwa na ulevi wa pombe kwa mwanajamii mlevi, familia yake na taifa kwa ujumla.en_US
dc.identifier.citationMagoma, J. (2017) Usawiri wa mhusika mlevi katika riwaya teule za Kiswahili. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/9159
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.titleUsawiri wa mhusika mlevi katika riwaya teule za Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
John Magoma.pdf
Size:
251.7 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: